Rais Vladimir Putin wa Urusi amepiga marufuku maandamano wakati
michezo ya Olimpiki ya msimu wa majira ya baridi kwa mwaka ujao
wa 2014.
Katika kufanikisha utekelezaji wa amri hiyo watu
mbalimbali kuanzia katika viwanja vya michezo, bandari, vituo vya
treni na vituo vya ukaguzi wa barabarani ambavyo vitakuwa maeneo
muhimu ya ukaguzi watakaguliwa na pamoja na mizigo yao.
Amri
hiyo ya rais ambayo imechapishwa katika gazeti la serikali
Rossiyskaya Gazeta imeweka maeneo maalumu ya usalama katika
jimbo la Sochi wakati wa michezo hiyo mwezi wa Februari katika
eneo la mapunziko la bahari Nyeusi.
Amri hiyo pia imeweka "ukanda
wa marufuku" kwa kuzuia kuingia katika maeneo ya michezo ya
Olimpiki pamoja na sehemu kubwa ya mji wa Sochi.
Aidha amri
hiyo imepiga marufuku kuvuka mpaka na kuingia katika eneo la waasi
la Abkhazia nchini Georgia, ambalo lipo umbali wa kilometa kadhaa
kutoka katika uwanja wa michezo ya Olimpiki.
Mpango wa Putin
umezuia maandamano yoyote ambayo hayahusiani na michezo ya
Olimpiki katika eneo husika kuanzia Januari 7 mpaka Machi 21,
2014.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment