Alitambulika rasmi kwenye game ya bongo fleva na ngoma iliyofahamika kwa jina kamwambie ukiwa ni mkono wa mteja wake wa zamani wa mitumba Bob Junior katika studio za Sharobaro Rec, huyu si mwingine ni asali ya warembo kama ambavyo anajiita mwenyewe Diamond platiunum.
Akipiga story na mboni masimba katika show yake ya Mboni show..........Diamond amefunguka kuwa mkwanja wa kwanza kukunja baada ya show ilikua shilingi 50,000 kwenye show ya fiesta mwaka 2009 pale kunako viwanja vya sayansi ambapo mnyamwezi Buster ryms alidondoka bongo.
Diamond amefunguka kuwa kwa sasa analipwa milion kumi kwa show moja ikiwa ni miaka mitatu tu toka alipwe 50,000!
Pia mkali huyo anayetamba na ngoma yake ya nataka kulewa aliodaiwa kuukopi beat ya artist Pasha na idea ya kiuno nyonga H.baba akusita kumtaja xgirlfreind wake Wema Sepetu kama mmoja wa wanawake waliofikisha hapo alipo.
Jina la Wema lilijitokeza pale mmoja wa washiriki wa kipindi hicho alipomtaka awataje wanawake watano ambao anadhani wamemfikisha hapo alipo, ndipo alipoanza kumtaja mama yake kisha Wema na Kidoti akafuatia kwa mbali baada ya kufikiria kwa muda mrefu
Hata hivyo Diamond amekataa kuwa na mahusiano na mwanamke yeyote kwa hivi sasa zaidi ya kuwa na marafiki tu tofauti na magazeti yanavyomuandika.
Mkali huyo pia amekiri kutomsaidia baba yake kwa sababu aliwatenga pamoja na mama yake way back kitendo kilichomkera.
Huyo ndio Platinum so mapromota uchwara jipangeni au msubirini chini pindi atakapodondoka na sijui ni lini coz kabla ya mwaka huu kumalizia atareleaz ngoma yake aliyofanya na j martin wa nigeria.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment