Haruna Chanongo akiwa ndani ya uzi wa timu ya taifa (taifa stars)
Winga Haruna
Chanongo wa Stand United ameikana Yanga baada ya kuwepo kwa taarifa kwamba
mchezaji huyo amesaini kuichezea timu hiyo.
Chanongo aliyekua
anaichezea Stand United kwa mkopo kutoka Simba alihusishwa kusajiliwa na Yanga pamoja
na mchezaji Dues Kaseke siku ya jumapili.
Akizungumza
na mtandao huu chanongo amesema hajasaini kuichezea yanga japo mazungumzo
yalianza kufanyika baina ya viongozi wa yanga na wakala wake lakini muafaka
bado haujafikiwa.
Kuhusu kwenda
kufanya majaribio kunako timu ya Tp mazembe Chanongo amesema majeruhi ndio sababu ya yeye
kushindwa kwenda DR Congo kufanya
majaribo.
Hata hivyo
kumekuwepo na taarifa nyingine kwamba Azam Fc wamejitosa kwenye kinyang’anyiro cha
kumtaka mchezaji huyo aliyemaliza mkataba na timu yake ya Simba.
0 comments:
Post a Comment