Katibu wa CCM Mkoa wa Iringa
Bw. Emanuel Mteming'ombe enzi za uhai wake
Mzee Teming'ombe akilia kwa uchungu kufuatia kifo cha kijana wake aliyekuwa katibu wa CCM mkoa wa Iringa Emanuel Mteming'ombe aliyefariki usiku wa kuamkia leo katika Hospital ya Rufaa ya mkoa wa Iringa
Waombolezaji wakiwa katika hospital ya rufaa ya mkoa wa Iringa katika maandalizi ya mwili wa aliyekuwa katibu wa CCM mkoa wa Iringa |
Na Francis Godwin, Iringa
KATIBU wa chama cha mapinduzi (CCM) mkoa wa Iringa Bw Emanuel Mteming'ombe amefariki dunia katika hospital ya mkoa wa Iringa.
Katibu huyo alikuwa amelazwa katika Hospital ya mkoa wa Iringa akisumbuliwa kwa ugonjwa athma kabla ya kufariki dunia usiku wa kuamkia leo.
Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Iringa Bi, Jesca Msambatavangu amethibitisha juu ya taarifa hiyo na kuwa taratibu za mazishi zinafanywa.
Taarifa zinasema mwili wa Maarehemu unatarajiwa kuombewa katika kanisa la RC Kichangani ama nyumbani kwake Gangilonga mjini Iringa kabla ya kuondoka mida ya saa 10 jioni kwenda Rujewa, Mbarali, mkoa wa Mbeya, kwa mazishi yanayotarajiwa kufanyika kesho saa 5 asubuhi.
Mungu ailaze roho yake mahali pema peponi.
Amina
0 comments:
Post a Comment