Baada ya kuvunjika kwa mchezo wa hatua ya 16 bora ya
michuano ya kombe la klabu bingwa amerika ya kusini kati ya Boca Juniors dhidi
ya wapinzani wake River Plate, Shirikisho la Soka la Amerika ya Kusini limetoa
adhabu kwa klabu ya Boca Juniors.
Boca Juniors imepewa adhabu ya kuondolewa katika michuano
hiyo baada ya mashabiki wa klabu hiyo kuwapulizia wachezahi wa River Plate dawa
iliyokuwa na pilipili machoni.
Adhabu hiyo haikuishia kwa Boca Juniors kuondolewa katika
hatua ya 16 bora pekee, bali pia kutozwa faini ya dola za kimarekani laki 2.
Mashabiki wa klabu ya Boca Juniors nao hawakuachwa katika
adhabu hiyo kwani nao wamefungiwa kuingia uwanjani katika michezo minne
inayokuja inayoihusu timu yao katika michuano ya Klabu Bingwa Amerika Kusini.
Wakati huohuo, klabu ya River Plate imeruhusiwa kuendelea
na robo fainali ya michuano hiyo na sasa watacheza na klabu ya Cruzeiro ya
nchini Brazil.
0 comments:
Post a Comment