Kocha wa klabu ya Arsenal Arsene Wenger amesema kuwa
hatostaafu baada ya msimu huu kumalizika.
Wenger kwa sasa ana miaka 65 na alijiunga katika klabu ya
Arsenal mwaka 1996 akitokea nchini Japana alipokuwa akifundisha klabu ya Nagoya
Grampus Eight.
Kocha Wenger amesema hajui maisha yake akistaafu
yatakuwaje huku akimuangalia kocha wa zamani wa Manchester United Sir Alex
Ferguson namna anavyoishi mara baada ya kustaafu.
Wenger anasema Ferguson anaonekana mtu mwenye furaha sana
mara baada ya kustaafu lakini najiuliza huwa anafanya nini kwa siku nzima?”
Wenger anaendelea kusema kuwa Ferguson ana bahati kwa kuwa anapenda mchezo
wa farasi hivyo anakuwa na muda mzuri wa kufanya mambo mengine katika mchezo
huo kama kujifunza na kupanda farasi.
Napenda Farasi lakini
siwezi kushindana katika mbio za Farasi kwani mimi ni mkulima amesema Wenger.
0 comments:
Post a Comment