Lionel Messi ameendelea kuwa mchezaji muhimu katika kikosi cha fc Barcelona baada ya jana kuifungia timu hiyo bao la ubingwa katika dakika ya 65 Barcelona ikipata ushindi wa 1-0
ugenini dhidi ya Atletico Madrid Uwanja wa Vicente Calderon mchezo wa La Liga.
ushindi huo dhidi ya timu ya Atletico ya Diego Simeone, umeiwezesha Barca kujihakikishia
taji la ubingwa wa La Liga, ambalo linakuwa taji la 23 katika historia
yao.
Lakini pia ni kama kulipiza kisasi kwa Simeone ambaye msimu uliopita alitangazia ubingwa wa La liga katika dimba la Nou Camp baada ya sare ya goli moja kwa moja, sasa jana barca katangazia ubingwa nyumbani kwa atletico pale Vicente Calderon.
0 comments:
Post a Comment