Mshambuliaji wa Southampton Sadio Mane
ameweka rekodi ya kufunga magoli matatu ya mapema katika historia ya Ligi Kuu
ya soka nchini England.
Mane amefunga magoli hayo ndani ya dakika 2 na sekunde
56.
Magoli hayo matatu ya Mane yanamfanya mchezaji huyo
kuvunja rekodi ya mshambuliaji wa zamani wa klabu ya Liverpool Robbie Fowler ya
kufunga magoli matatu ndani ya dakika 4 na sekunde 33.
Fowler alifunga magoli hayo katika mchezo kati ya
Liverpool dhidi ya Arsenal.
Ila wawili hao wanaweza wasijivunie sana kwani katika
historia ya soka nchini England, hat
trick ya mapema kabisa ni ile aliyofunga James Hayter katika mchezo wa Ligi
daraja la pili mwaka 2004 kati ya timu yake ya AFC Bournemouth na timu ya Wrexham.
Katika mchezo huo Hayter alitumia muda wa dakika 2 na
sekunde 20 kufunga magoli matatu.
0 comments:
Post a Comment