Afisa habari wa Coastal Union Oscar Assenga
MKUTANO Mkuu wa Dharura wa Wanachama wa Klabu ya Coastal Union unatarajiwa kufanyika kesho Mei 17 mwaka huu kwenye ukumbi wa Bwalo la
Polisi Mkoani Tanga.
Sababu za Mkutano huo kufanyika katika Ukumbi la Polisi Mesi ni
kutokana na makao makuu ya klabu ya Coastal Union kuendelea mchakato wa uandikishaji wa vitambulisho vya Taifa na upigaji picha wananchi
kwa ajili ya vitambulisho hivyo.
Akizungumza leo,Ofisa Habari wa Coastal Union,Oscar Assenga alisema maandalizi ya mkutano huo yanaendelea vizuri na unafanyika kufuatia vikao vya maridhiano ya Uhakikiwa wanachama wa Klabu ya Coastal Union ulioongozwa na Mjumbe wa Kamati
ya Utendaji ya Shirikisho la soka nchini (TFF) Ahmed Iddi Mgoyi.
Ambapo alisema baada ya kumalizika vikao hivyo,Katibu Mkuu wa TFF, Mwesigwa Selestine aliiandikia barua Klabu ya Coastal Union akiiagiza klabu hiyo kuitisha mkutano mkuu wa dharura wa wanachama tarehe 17 Mei mwaka 2015.
Alisema kuwa matokeo ya maamuzi haya yamepatikana baada ya kikao cha usuluhishi cha amani kilichoongozwa na Mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya TFF, Ahmed Iddi Mgoi aliyekuwa ameongozana na Makamu Mkurugenzi wa Sheria na Uanachama shirikisho la soka nchini (TFF) Eliud Peter Mvella kilichofanyika April 13 mjini hapa.
Aidha alisema kuwa tayari shirikisho la soka nchini (TFF) ilishatuma
orodha tatu za majina Wanachama stahiki,Wanachama waliobainika kuwa wanadosari na inabidi wathibitishwe na wanachama stahiki.
Orodha nyengine ni waombaji wapya wa wa uanachama watakaohakikiwa na wanachama stahiki ambapo utaratibu huo ndio ulioagizwa kutumika .
Hata hivyo alisema kuwa orodha zote zimekwisha kubandikwa kwenye ubao wa Matangazo wa Klabu ya Coastal Union tayari kwa ajili ya mkutano huo wa kesho
Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano Coastal Union.
Saturday, May 16, 2015
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment