Main Menu

Tuesday, November 19, 2013

HIVI NDIVYO SAFARI YA DKT. MVUNGI ILIVYOHITIMISHWA KIJIJI KWAO CHANJALE MWANGA KILIMANJARO


Askofu Damian Dallu wa Kanisa Katoliki Jimbo la Geita akiongoza ibada ya mazishi ya aliyekuwa Mjumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba marehemu Dkt. Sengondo Mvungi katika makaburi ya familia kijijini Chanjale wilaya ya Mwanga mkoani Kilimanjaro jana, Novemba 18, 2013.
Mke wa aliyekuwa Mjumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba marehemu Dkt. Sengondo Mvungi, Bi. Anna Mvungi akiweka shada la maua katika kaburi la mume wake wakati wa mazishi.
Waziri wa Uchukuzi Dkt. Harrison Mwakyembe na Mwenyekiti wa NCCR-Mageuzi James Mbatia wakiweka shada la maua katika kaburi la aliyekuwa Mjumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba Dkt. Sengondo Mvungi wakati wa mazishi kijijini Chanjale wilaya ya Mwanga mkoani Kilimanjaro .
Jeneza lenye mwili wa aliyekuwa Mjumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba Dkt. Sengondo Mvungi likishushwa kaburini .
Waziri Mkuu Mizengo Pinda, mkewe Mama Tunu, Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba Jaji Joseph Warioba na viongozi wengine wakifuatilia ibada ya mazishi ya aliyekuwa Mjumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba Dkt. Sengondo Mvungi.
Familia ya aliyekuwa Mjumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba Dkt. Sengondo Mvungi ikifuatilia ibada ya mazishi iliyofanyika katika kijiji cha Chanjale wilaya ya Mwanga mkoani Kilimanjaro jana.
Askofu Mkuu wa Kanisa Katoliki Jimbo Kuu la Arusha Josephat Lobullu (kulia) na Askofu wa Jimbo la Same Rogath Kimaryo wakiongoza ibada ya mazishi ya aliyekuwa Mjumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba Dkt. Sengondo Mvungi. Ibada hiyo ilifanyika katika kijiji cha Chanjale wilayani Mwanga mkoani Kilimanjaro na kuhudhuriwa pia na Askofu Damian Dallu (katikati) wa Jimbo la Geita.

na michuziblog

0 comments:

Post a Comment