Kiungo wa Arsenal Jack Wilshere akionekana dhahiri akionyesha dhihaka ya kidole cha kati uwanjani Etihad
|
Jack
Wilshere wa Arsenal amekutana na adhabu ya chama cha soka nchini
England (FA) ya kusimama mchezo mmoja, kufuatia kuonyesha dhihaka ya
dole la kati kwa mashabiki wa Manchester City wakati wa mchezo
waliopoteza kwa kichapo takatifu cha mabao 6-3 mchezo ulichezwa katika
dimba la ugenini la Etihad.
Chama cha soka cha England kimepitia taarifa ya mchezo mzima ya mwamuzi Martin
Atkinson kabla ya kuzindua kusikiliza kesi dhidi ya Wilshere
kufuatia picha za televisheni kumuonyesha akiinua kidole cha kati kuelekea kwa mashabiki wa timu mwenyeji.
Meneja wa Arsenal Arsene Wenger hapo kabla alikaririwa akisema klabu yake itakubaliana na adhabu hiyo ya FA kwa kiungo wake.
Wilshere amepewa mpaka kesho jioni kutoa neno lolote kuhusiana na adhabu hiyo.
Taarifa ya FA imesomeka
'Kiungo wa Arsenal Jack Wilshere ameadhibiwa na FA kwa kosa la kutukana kwa kutumia dhihaka.
'Adhabu
inakuja kufuatia kuyonyesha dhihaka hiyo wakati wa mchezo baina ya
Manchester City na Arsenal uliochezwa uwanja wa Etihad Jumamosi ya
Disemba 14. Tukio hilo halikuonwa na waamuzi wa mchezo lakini ni kwa
kupitia video ya mchezo husika.
'Wilshere
amehadhibiwa wakati huu ambapo FA ikiwa chini ya mradi wake wa kupiga
vita matukio yasiyokuwa yakistaarabu uwanjani katika michezo ya Premier
League.
'katika
mpango wa sasa wa FA endapo kuna tukio lolote ambalo halikuonekana na
waamuzi, timu ya watu watatu itaundwa na FA kupitia tukio husika na na
kusahauri kwa tukio ambalo pengine mwamuzi alipaswa kutolea maamuzi kwa
wakati husika.
Wilshere hakuwa katika kiwango kizuri siku ya tukio mchezo uliochezwa Etihad
Mshambuliaji
wa Liverpool Luis Suarez aliwahi kufungiwa mchezo mmoja na kipigwa
faini ya pauni £20,000 na kisha kuonywa kutokufanya hivyo hapo baadaye
kufuatia dhidhaka kuelekea kwa mashabiki wa uwanja wa nyumbani wakati
akitoka uwanjani katika mchezo wa kichapo cha bao 1-0 kutoka kwa Fulham
Disemba 2011.
Euro
2000: David Beckham akiwa kijana alionyesha dhihaka ya kidole cha kati
kwa mashabiki baada ya kichapo cha timu ya taifa ya England kutoka kwa
Ureno cha mabao 3-2
Huko nyuma Luis Suarez wa Liverpool alionyesha dole la kati kwa mashabiki wa Fulham na kisha kusimamishwa kwa mchezo mmoja.
0 comments:
Post a Comment