Main Menu

Tuesday, December 17, 2013

UFARANSA KUIDHINISHA DAWA ZA KUJIUA

Jopo lililoundwa  na  rais  wa  Ufaransa  Francois Hollande limependeleza  kuhalalishwa  kwa  kujiua kwa  kutumia dawa  ya  usingizi. 

Jopo  la  watu  18, lililokuwa  na wawakilishi  kutoka  umma  wa  Ufaransa, limesema  jana kuwa msaada  wa  madaktari  wa  kuweza  kujiua  uwe halali  katika  hali  ya kuwa  mtu  atakuwa  mgonjwa  kiasi kwamba  hana  matumaini  ya  kuishi  tena. 

Mapendekezo hayo  yanapingana  na  kamati  ya  maadili  ya  kitaifa nchini  Ufaransa , ambayo  inasema  madaktari  hawapaswi kuwasaidia  wagonjwa  ambao  hawana  matumaini  ya kuishi  kujiua. Hollande  ameahidi  kuitisha  mjadala  wa kitaifa  kuhusu  suala  hilo. 

Hii  inakuja  baada  ya  baraza la  seneti  la  Ubelgiji  mapema  wiki hii  kuidhinisha mpango  wa  kurefusha  sheria  ya  matumizi  ya  dawa  ya kujiua  'Yuthanesia' kwa  wagonjwa  ambao  ni  watoto ambao  hawana  nafasi  tena  ya  kuishi.

0 comments:

Post a Comment