Timu
ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars) itacheza mchezo wake wa kwanza wa
kombe la COSAFA siku ya jumatatu dhidi ya Swaziland katika uwanja wa
Royal Bafokeng pembeni kidogo ya jiji la Rustenburg kuanzia majira ya
saa 1:30 jioni kwa saa za Afrika Kusini.
Awali
michezo ya kundi B ilikuwa ifanyike katika uwanja wa Olympia Park,
lakini waandaji wa michuano ya COSAFA Castle wamesema kutokana na sababu
zilizopo nje ya uwezo wao michezo hiyo imeshindikana kufanyika katika
uwanja huo.
Uwanja
wa Royal Bafokeng ni miongoni mwa viwanja viliyotumika katika Fainali
za Kombe la Dunia 2010 chini Afrika kusini, ukiwa na uwezo wa kubeba
watazamaji 42,000 huku timu ya Platinum Stars iliyopo Ligi Kuu
ikiutumia kama uwanja wake wa nyumbani.
Leo
asubuhi Taifa Stars imefanya mazoezi katika uwanja wa shule ya
Rustenburg chini ya kocha mkuu Mart Nooij, na wachezaji wote wapo katika
hali nzuri kuelekea katika mchezo huo wa jumatatu.
Kesho
jioni Taifa Stars ifanya mazoezi saa jioni katika uwanja wa Rolay
Bafokeng kwa ajili ya kuuzoea uwanja kabla ya mchezo wenyewe dhidi ya
Swaziland.
Akiongelea
hali ya hewa, kocha mkuu wa Taifa Stars Mart Nooij amesema vijana wake
wanaendelea kuizoea hali ya hewa, japokuwa kuna baridi hakuna mchezaji
aliyeshindwa kufanya mazoezi kutokana na hali ya hewa.
0 comments:
Post a Comment