Mwenyekiti wa klabu ya Young Africans Bw. Yusuf Manji amewaomba
wanachama, wapenzi na washabiki wasivunjike moyo kwa matokeo ya jana ya
mchezo wa kirafiki dhidi ya ya Simba SC, mechi iliyochezwa katika dimba
la Uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam.
Akiongea na waandishi wa habari makao makuu ya klabu ya Yanga
makutano ya mitaa wa Twiga/Jangwani Manji amesema anajua wanachama, na
wapenzi wameumia sana hakuna aliyefurahishwa na matokeo ya kufungwa
mabao 3-1 lakini isiwakatishe tamaa uongozi unafanyia kazi mapungufu
yaliyojitokeza.
"Mechi ya jana ilikuwa ni bonanza, ndio maana
hapakuwa na timu iliyopata pointi katika mchezo huo zaidi ya
kusherehekea, sisi tumepata zawadi ya milion 98 wakati wenzetu Simba SC
wamepata milion 1, hivyo zaidi sisi tumeendelea kuimarika kiuchumi zaidi
wenzetu wameishia kusherehekea" alisema Manji.
Aidha
amesema wachezaji zaidi ya tisa wa Yanga hawajapata muda wa kupumzika
tangu mwezi Novemba baada ya kumalizika kwa mzunguko wa kwanza wa Ligi
Kuu kwani walijiungana timu za Taifa na wamekua huko kwa takribani mwezi
mzima bila kupumzika tofauti na wenzetu Simba SC ambao hawana wachezaji
wengi timu ya Taifa.
Manji pia alisema anawapa hongera timu ya
Simba SC kwa kushinda bonanza la jana, amesema mchezo wa jana walicheza
vizuri hivyo wanastahili pongezi kwa hilo.
Akijibu maswali ya
waandishi wa habari juu ya mapungufu yaliyojitokez katika mchezo wa
jana, amesema kamati husika inayafanyia kazi na kwa kuwa yeye anasafiri
leo kwenda nje ya nchi majukumu yote amemkabidhi makamu mwenyekiti
Clement Sanga mpaka yeye atakaporejea.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment