Hatua ya mtoano ya Ligi ya kikapu nchini Marekani maarufu
kama NBA imeendelea alfajiri ya leo kwa
michezo miwili.
Timu ya Golden State Warriors imekata tiketi ya kucheza
fainali ya kanda ya Magharibi mara baada ya kuifunga timu ya Memphis kwa pointi
108 kwa 95.
Katika mchezo huo mchezaji wa Golden State Warriors
Stephen Curry alifunga pointi 32 huku Marc Gasol kwa upande wa Memphis akifunga
pointi 21.
Kwa matokeo hayo, Golden State Warriors wanamsubiri
mshindi kati ya Houston Rockets na LA Clipers katika fainali ya kanda ya
Magharibi.
Kwa upande wa kanda ya Mashariki timu ya Atlanta imefuzu
fainali ya kanda hiyo mara baada ya kuifunga timu ya Washington Wizards alfajiri
ya leo kwa pointi 94 kwa 91.
0 comments:
Post a Comment