Timu ya Taifa ya Tanzania
(Taifa Stars) kesho itashuka uwanjani katika mchezo wake wa kwanza wa
kombe la COSAFA dhidi ya Swaziland katika uwanja wa Royal Bafokeng pembeni
kidogo ya jiji la Rustenburg kuanzia majira ya saa 1:30 jioni kwa saa za Afrika
Kusini.
Uwanja wa Royal Bafokeng ni miongoni mwa
viwanja viliyotumika katika Fainali za Kombe la Dunia mwaka 2010 nchini Afrika
kusini, ukiwa na uwezo wa kubeba watazamaji 42,000 huku timu ya Platinum
Stars iliyopo Ligi Kuu ya PSL ikiutumia kama uwanja wake wa nyumbani.
Leo jioni Taifa Stars imefanya mazoezi katika
uwanja wa Royal Bafokeng kwa ajili ya kuuzoea uwanja kabla ya mchezo wenyewe
dhidi ya Swaziland.
0 comments:
Post a Comment