HATIMAYE
mshambuliaji Emmanuel Arnold Okwi amewasili Uwanja wa Ndege wa
Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA), Dar es Salaam jioni hii tayari
kuanza kuutumikia Mkataba wake wa miaka miwili ndani ya klabu ya Yanga
SC ya Tanzania.
Okwi
alitua kwa ndege ya RwandaAir Saa 9:55 jioni na kulakiwa na viongozi na
wapenzi kadhaa wa timu hiyo JNIA kabla ya kupakiwa kwenye gari ndogo
aina ya saluni alilokuwa akiendesha Mwenyekiti wa Kamati ya Mashindano
ya Kimataifa ya Yanga, Seif Ahmed ‘Magari’ na kuondoka.
Okwi
alitokea geti la wageni maalum la JNIA na kusindikizwa na Polisi huku,
umati wa mashabiki wa Yanga ukimshangilia na kumfanya atoke kwa taabu
hadi kupanda gari.
Mara
tu baada ya kutoka nje ya JNIA, Okwi alisema; “Nimekuja Yanga kufanya
kazi,” na alipoulizwa kuhusu utata wa usajili wake, akasema; “Mimi
nimekuja kufanya kazi, hayo mengine, mamlaka husika zitajua,”alisema
Okwi aliyekuwa amevalia jezi nambari 25 ya Yanga.
Kwa
upande wake, Mwenyekiti wa Kamati ya Mashindano ya Yanga, Abdaollah
Ahmed Bin Kleb alisema kwamba mchezaji huyo anakwenda moja kwa moja
kambini, Protea Hotel kuungana na wenzake tayari kwa mchezo wa Jumamosi
wa Nani Mtani Jembe dhidi ya mahasimu, Simba SC.
Simba
na Yanga zitamenyana Jumamosi katika mchezo ambao iwapo dakika 90
zitamalizika kwa sare, mikwaju ya penalti itaamua mshindi.
Mchezo
huo, unaoandaliwa na wadhamini wa klabu hizo, Kampuni ya Bia Tanzania
(TBL) kupitia bia ya Kilimanjaro Premium Lager, unatarajiwa kuchezeshwa
na refa Ramadhan Ibada ‘Kibo’ kutoka Zanzibar, atakayesaidiwa na
Ferdinand Chacha wa Bukoba na Simon Charles kutoka Dodoma, wakati refa
wa akiba atakuwa Israel Nkongo wa Dar es Salaam na mtathimini wa waamuzi
ni Soud Abdi wa Arusha.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment