Main Menu

Monday, May 25, 2015

ROGER FEDERER AVAMIWA UWANJANI



Mcheza tenisi Roger Federer amekosoa ulinzi uliopo katika mashindano ya wazi ya Tenisi yanayofanyika nchini ufaransa baada ya mtazamaji mmoja kukimbilia uwanjani na kujaribu kupiga picha na mchezaji huyo raia wa Uswisi.

Tukio hilo limemsikitisha sana mcheza tenisi huyo namba mbili kwa ubora duniani kwa sababu ya kuhofia usalama wake.

Mvamizi huyo ameondolewa na walinzi wa uwanjani, ingawa tayari  ameshafanikiwa kumuomba Federer akae mkao wa kupiga picha na kumpiga picha.

Baada ya tukio hilo Federer amesema kuwa  "Sifurahii jambo hili, imetokea pia wakati wa mazoezi ambapo mtoto mmoja amefika uwanjani kupiga picha na mimi na kisha watatu zaidi wakaja"amesema  Federer.

Tukio hilo limetokea katika mchezo ambao Federer alipata ushindi wa seti 6-3 6-3 6-4 dhidi ya Mcolombia Alejandro Falla.

Hilo si tukio la kwanza kwa Federer kuvamiwa na shabiki na kuombwa kupiga picha.

Mwaka 2009, tukio kama hilo limewahi kumtokea nyota huyo kwa kuvamiwa na mmoja kati ya mashabiki katika mchezo wa fainali kati yake Federer na Robin Soderling.

Mwaka 2013 pia tukio kama hilo lilimtokea katika mchezo kati yake na Rafael Nadal.

Federer ametoa wito kwa niaba ya wacheza Tenisi wote wanaoshiriki michuano hiyo ya Ufaransa kuomba idara ya ulinzi ya michuano hiyo inayoongozwa na Mkurugenzi Gilbert Ysern kuimarisha ulinzi kwa wachezaji wote wanaoshiriki michuano hiyo.

0 comments:

Post a Comment