Leo
Rais wa Baraza la Vyama vya Mpira wa Miguu Afrika Mashariki na Kati (CECAFA),
Leodegar Tenga na mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya Shirikisho la Mpira wa Miguu
Afrika (CAF) akiwa na Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF),
Jamal Malinzi wamezungumzia uchaguzi wa CAF na FIFA.
Rais
Tenga ameishukuru familia ya TFF kwa kumuunga mkono katika kugombea tena nafasi
ya ujumbe wa Kamati ya Utendaji ya CAF katika uchaguzi utakaofanyika Aprili 7
mwaka huu Cairo. Tenga ni mgombea pekee wa nafasi hiyo kwa Kanda ya Afrika
Mashariki na Kati.
Pia
Rais Tenga amezungumzia msimamo wa bara la Afrika uliowekwa katika Mkutano Mkuu
wa CAF uliofanyika mwaka jana jijini Sao Paulo, Brazil kuwa wanachama wote wa
CAF watamuunga mkono Rais wa sasa wa FIFA anayetetea nafasi yake katika
uchaguzi utakaofanyika Mei mwaka huu jijini Zurich, Uswisi.
Vilevile
Mkutano Mkuu wa CECAFA uliofanyika Desemba 2014 jijini Nairobi, Kenya
ulipitisha azimio la kumuunga mkono Joseph Sepp Blatter katika uchaguzi wa FIFA.
Katika
mkutano huo, Rais wa TFF, Jamal Malinzi ametoa tamko rasmi kuwa kwa niaba ya
TFF atampigia kura Joseph Sepp Blatter.
0 comments:
Post a Comment