Siku moja baada ya Baraza la Soka Afrika Mashariki na Kati (CECAFA) kuziteua timu za URA, Elite Sport ya Chard na Rayon Sports ya Rwanda
kuziba nafasi za timu za Tanzania, Serikali jana imetangaza kuziruhusu timu hizo kushiriki michuano hiyo iliyopangwa kuanza Jumanne ijayo Juni 18
Durfur nchini Sudan.
Naibu Waziri wa Habari Utamaduni na Michezo Amosi Makalla aliiambia jana kuwa serikali ya Sudan imewahakikishia kwa maandishi kuzipa
usalama timu za Tanzania zitakazoenda kushiriki michuano hiyo ambayo Yanga ni bingwa mtetezi.
"Tulikuwa tunakataa kwa vile hatukupata taarifa rasmi ya maandishi kutoka serikali ya Sudan kutuhakikishia usalama wa watu wetu kuanzia uwanja
wa ndege zitakapotua, zitakapokuwa Khatoum, ulinzi wa kuzitoa Khatorm hadi Durfur na hoteli watakazofikia, lakini jana imetuhakikishia usalama
na siku zote Chama cha Soka cha Sudan ndio kilichokuwa kikituambia kuna usalama tusingeweza kuamini, lakini kwa vile tumepata udhibitisho wa
serikali timu ruksa kwenda."alisisitiza
"Timu zote zilikuwa zinajiandaa na mashindano ni tarehe 18 kama zinataka kwenda ziende, na hao Cecafa kama wameteua timu nyingine iyo ni juu
yao."
Makala ambaye juzi alitoa msimamo wa serikali akipigilia nyundo kauli ya Waziri wa Mambo ya Nje Benard Membe alisema serikali ndio inajua hali
ya usalama ya Durfur ilivyo hivyo haiwezi kuziruhusu timu za Simba, Yanga na Super Falcon ya Zanzibar zikashiriki michuan hiyo.
Hata hivyo viongozi wa Simba na Yanga jana walipoulizwa kuhusiana na suala hilo walionekana kuduwazwa kwani hawakuwa na taarifa yoyote ya
serikali au TFF ikiwajulisha juu ya jambo hilo, huku timu zote zilishatoa msimamo wa kutoshiriki michuano hiyo baada ya kuambiwa Durfur si
salama.
Laurance Mwalusako Katibu mkuu wa Yanga "Ili suala kuna mgongano wa mambo mengi, mpaka sasa hivi klabu hatuna taarifa zozote, na isitoshe sisi jana tumevunja kambi na tumewapa wachezaji wetu mapumziko ya wiki mbili, hata hivyo tukipata
tutakaa na kujadili kama tushiriki au la."
Ismail Aden Rage Mwenyekiti Simba "Mi sina habari zozote nipo na Waziri huku (Dom)mbona hajaniambia chochote, ngoja akishaniambia ndio tunaweza
kutoa msimamo wetu lakini kwa sasa hatuna taarifa zozote."
Hata hivyo licha ya serikali kuziruhusu hadi jana mchana Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), kupitia kwa katibu wake Angetile Osiah alisema bado
hawajapata taarifa rasmi zaidi ya taarifa ya juzi ambayo serikali waliituma kwa katibu wa Cecafa Nicholaus Musonye ya kutaka wadhibitishiwe kama
kweli kuna usalama.
"Rais Tenga juzi aliwatumia barua ya Waziri wa Michezo wa Durfur ya kuwahakikisha usalama wa kutosha kwa timu zetu, zaidi ya hiyo hatujapata
taarifa nyingine mpaka sasa hivi." alisema Osiah.
0 comments:
Post a Comment