Kampuni
ya Bia Tanzania (TBL) chini ya Bia yake ya Kilimanjaro, inataraji
kuanza rasmi tamasha kubwa la muziki lijulikanalo kama ‘Kili Music Tour’
wikiendi hii katika mji wa Dodoma.
Tamasha
hii kubwa linatarajiwa kuanza siku ya Jumamosi ya tarehe 22 Juni,
2013 mjini Dodoma kwenye viwanja vya Jamhuri na litajumuisha wasaniii 8
ambao ni Ally Kiba, Ommy Dimpoz, Professor J, Ben Pol, Lady Jay Dee,
Lynex, Roma na Kala Jeremiah.
Mwaka
huu Bia ya Kilimanjaro imebadilisha utaratibu wa tamasha hili la muziki
ambalo lilikuwa linajulikana kama KTMA Winners Tour na lilikuwa
likijumuisha wasanii walioshinda tuzo za Kilimanjaro Tanzania Music
Awards pekee.
Mwaka
huu bia ya Kilimanjaro imebadilisha jina la tamasha kuwa Kili Music
Tour na litashirikisha wasanii wote kwa ujumla na sio washindi wa tuzo
za KTMA pekee.
“Kili
Music Tour imepanua wigo wake kwa kushirikisha wasanii walioshinda
tuzo, wasanii waliokuwa kwenye mapendekezo ya tuzo na wasanii ambao
hawakushiriki kabisa kwenye tuzo lakini wako juu kwenye tasnia ya muziki
nchini.
Hii
ni kwenye kuhakikisha kuwa mashabiki wa muziki wanapelekewa wasanii
wanaowapenda kwenye mikoa yako bila kubagua. Mwaka huu matamasha
yameongezeka kutoka sita mwaka jana na kuwa nane.
Kili
inaelewa ni jinsi gani watanzania wanajivunia mambo ya kitanzania kama
muziki wetu wa bongo flava, dansi yetu ya kiduku, kandanda letu lenye
ushabiki wa simba na yanga, lugha yetu ya kipekee na bia yetu ya
Kilimanjaro inayowapa bonge la kiburudisho .
Ndio
maana tumeongeza wigo wa Tamasha kama ishara ya shukurani kwa jinsi
watanzania wanavyojivunia mambo ya kikwetu kwetu.” Alisema Bwana George
Kavishe Meneja wa bia ya Kilimanjaro.
Msanii
aliyebobea wa bongo flava ajulikanaye kama Kala Jeremiah naye alisema “
mwaka huu mashabiki wategemee kupata vionjo ambavyo hawajawai kuviona
kwani mimi na wasanii wenzangu tumejipanga kikamilifu kuhakikish kuwa
hatuwaangushi mashabiki wetu na kuwa tunawapa bonge la kiburudisho!”
0 comments:
Post a Comment