Main Menu

Wednesday, June 19, 2013

WASHIRIKI MISS IRINGA WALALAMIKIA UFINYU WA ZAWADI ZILIZOTOLEWA NA WAANDAAJI

Tano bora ya Redds Miss Iringa 2013 iliyofanyika hivi karibuni katika ukumbi wa Highlands

Baaadhi wa washiriki wa Redds miss Iringa 2013 wamelalamikia ufinyu wa zawadi zilizotolewa  na waandaaji wa shindano hilo kwa madai kuwa gharama walizotumia hazilingani na anachopata mshindi.

Wakizungumza na mtandao huu baadhi wa warembo hao walioshiriki shindano hilo lililofanyika tarehe 14 june mwaka huu katika ukumbi wa highlands wamesema zawadi iliyotolewa kwa mshindi wa kwanza hadi wa tatu na kifuta jasho kwa washiriki wengine ni kidogo mno.

Katika shindano hilo mshindi wa kwanza alipata kiasi cha shilingi laki tano taslimu, Mshindi wa pili laki tatu taslimu na Mshindi wa tatu laki mbili taslimu huku washiriki wengine waliobaki wakiambulia kifuta jasho cha shilingi elfu hamsini kila mmoja.

Akijibu malalamiko hayo mratibu wa miss Iringa Doss Magambo amesema zawadi zilizotolewa ni sahihi kutokana na wadhamini waliojitokeza.

Hata hivyo magambo amesema udogo wa zawadi unaonekana kutokana na zawadi kutolewa kwa washindi watatu wa juu, wakati ilipaswa zawadi kuwa moja tu kwa mshindi kama ilivyo kwa miss Tanzania.

Aidha magambo ametoa wito kwa wafanya biashara na makampuni mkoani iringa kujitokeza kwa wingi pindi zinapotangazwa nafasi za udhamini wa shindano hilo ili kuboresha zawadi na shindano hilo kwa ujumla.

0 comments:

Post a Comment