Kibaka akiendelea kupata kichapo............
Mmoja wa vijana akionyesha mkono ukiwa umechafuka damu kutokana na kutoa kipigo kwa kibaka huyo
kamata kamata mwizi mitaaniwananchi mitaani wakiwa na dhana zao za jadi
Hapa ilikua kwenye kilabu kimoja cha pombe za kienyeji wakimtafuta kibaka mwngine
Wananchi wakimpeleka mmoja wa vibaka hao kituo cha polisi huku polisi wakijitahidi kumuwekea ulinzi asiendelee kupigwa
Wananchi mkoani
iringa hii leo wemeingia mitaani kuwatafuta, kuwapiga, na kuwakamata na
kuwapeleka polisi vibaka wanaodaiwa kuwa wapiga nondo nyakati za usiku.
Hatua hiyo
imekuja baada ya kijana mmoja anayefahamika kwa jina la salmu kuvamiwa na
kuporwa na vibaka hao siku ya jumamosi ambapo aliporwa simu pamoja na fedha
akiwa na wenzake wawili.
Baada ya
kijana huyo kupona majeraha aliyoyapata alifanikiwa kumpata mmoja wa kijana
aliyempora kwa kuwa alimkariri usiku ule na kuwajulisha vijana wenzake ndipo
walipomvamia na kumpa kichapo cha maana na kuwataja wenzake walioshirikiana nae
usiku ule.
Kundi hilo
la wananchi lilifanikiwa kuwakamata vijana watatu huku msako ukiendelea kwa
kijana mwingine ili kukamilisha list ya waliotajwa.
Hatua hiyo
imekuja baada ya kukithiri kwa vitendo vya upigaji nondo klatika maeneo ya manispaa ya iringa zaidi kata za kitanzini na
mivinjeni.
0 comments:
Post a Comment