mkuu wa wilaya ya kilolo gerald guninita
UTANGULIZI
Wilaya ya Kilolo ina eneo la kilometa za mraba zipatazo 7,881 ikiwa Kilometa za mraba 5,331 zinafaa kwa
Kilimo na shughuli za Ufugaji, eneo la
Kilometa za mraba 2,550 ni eneo la misitu
ya asili, milima na hifadhi za wanyama. Sensa
ya watu na makazi ya mwaka 2012 ilionyesha Wilaya ilikuwa na watu 218,227 kati yao wanawake
ni 112,622 na wanaume
ni 105,605 .Wilaya ya Kilolo kiutawala
ina Jimbo 1 la Uchaguzi (Jimbo la
Kilolo), Tarafa 3, Kata 22, Vijiji 106, Vitongoji 555 na Kaya 51,455.
HALI YA ULINZI NA USALAMA
Kwa kipindi hiki cha January - April 2013, Hali ya ulinzi na usalama katika maeneo
yote ya Wilaya inaendelea kuwa ya amani na utulivu .Hakuna matukio makubwa
yaliyosababisha wananchi kushindwa kuendelea na shughuli za maendeleo na
kijamii. Matukio madogomadogo ya uhalifu yaliendelea kudhibitiwa na vyombo vya
dola kikamilifu.
UTAWALA BORA
Wilaya imeendelea kuendesha shughuli zake za kiutawala na
kisiasa ambapo mambo yafuatayo yamefanyika
·
Vyama vya siasa vimeendelea na
shughuli zao kwa amani na utulivu.
·
Kuendesha vikao vya kamati
mbalimbali zilizoko Wilayani kama ifuatavyo:- Kikao cha kamati ya wataalamu wa Wilaya, kamati ya Fedha mipango na utawala, kamati ya Elimu Afya na
maji, kamati ya uchumi , ujenzi na mazingira, kamati ya maadili ya Wilaya na
Baraza la madiwani tarehe 24/04/2013
·
Kikao cha kamati ya maadili ya
mahakama Wilaya kimefanyika tarehe 14/03/2013 na kuazimia kuwa elimu itolewe kwa wananchi juu ya umuhimu
wa kamati hii na taarifa hii iwafikie wananchi
kupitia Waheshimiwa Madiwani na watendaji, ambapo katika kikao cha
Baraza la madiwani 24/04/2013 ujumbe huo
ulitolewa katika Taarifa ya Serikali na Mkuu wa Wilaya.
·
Serikali iliendelea kuwahimiza
viongozi wa Serikali za Vijiji kuhakikisha mikutano mikuu ya Vijiji inafanyika
kila baada ya miezi mitatu na kuwasomea wananchi mapato na matumizi (Tunategemea
kupokea mihtasari hiyo hivi karibuni kama ilivyoagizwa)
·
Uzinduzi wa Mahakama ya Mwanzo
Kilolo umefanywa na Jaji Kiongozi wa Mahakama Kuu ya Tanzania Mh. Fakih Jundu tarehe 30 April 2013 ikiwa ni moja ya
utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya 2010, Ibala ya 187. Jengo hili la kisasa
la Mahakama hii limegharimu jumla ya Shilingi Milioni Mia mbili thelathini laki moja thelathini na saba elfu mia mbili themanini na senti
arobaini (Tsh. 230, 137,280.40/=).
TAARIFA
YA UTEKELEZAJI WA SHUGHULI ZA MAENDELEO KWA KIPINDI CHA JANUARI – APRIL 2013
Wilaya
ya Kilolo Kwa mwaka wa fedha wa 2012/2013 iliidhinishiwa shillingi Bilioni sita
arobaini na tatu milioni laki tatu themanini na mbili elfu, miambili sitini na
tatu na senti kumi na tano(6,043,382,263.15/=)
ikiwemo bakaa ya Shilingi Bilioni moja milioni mia moja kumi na moja na thelathini na tisa elfu mia
tano themanini na mbili na senti thelathini na tatu ( 1,111,039,582.33) ya mwaka 2011/2012 kwa ajili ya utekelezaji wa
Miradi ya Maendeleo.Hadi kufikia mwezi April 2013 Halmashauri ya Wilaya ya
kilolo Imepokea Jumla ya Tshs. Bilioni nne
milioni mia moja thelathini na sita laki mbili kumi na tatu elfu mia sita ishirini na nane
na senti sitini na tatu (4,136,213,628.63) ikijumuishwa na
bakaa ya mwaka 2011/2012.Jumla ya fedha zilizotumika kwa kipindi cha Julai hadi April, 2013 ni Tshs.
Bilioni mbili milioni mia nne themanini
na tisa laki tatu na sita elfu mia nne hamsini na moja na senti tisini na tisa (2,489,306,451.99)
Kwa ajili ya utekelezaji wa miradi
mbalimbali ya maendeleo.Hivyo inafanya Wilaya kuwa na bakaa ya Tshs.
Bilioni moja milioni mia sita arobaini na sita laki tisa na saba elfu mia moja sabini na sita na senti sitini na nne (1,646,907,176.64) za miradi ya
Maendeleo. Aidha kwa kipindi cha Januari hadi April 2013 Wilaya imetekeleza Miradi
mbalimbali ya Maendeleo kama ilivyoanishwa
kisekta hapa chini.
IDARA YA UJENZI
Jumla ya Tshs.Bilioni moja milioni mia saba na kumi
laki tano hamsini na moja elfu (1,710,551,000/=) zimetengwa katika utekelezaji wa shughuli za
Ujenzi ikiwa hadi April,2013 imetumia jumla ya Tshs. Milioni mia nne na kumi
laki nane themanini elfu mia nne.(410,880,400/=) katika kutekeleza
shughuli mbalimbali zikiwemo :-Matengenezo ya kawaida (Routine Maintenance) kwa
jumla ya Km.30 kama ifuatavyo;-
·
Matengenezo ya kawaida na kudumu
barabara ya Ilula Mjini KM 7 na Kazi
inaendelea
·
Matengenezo ya kawaida na kudumu
barabara ya Ihimbo - Kising'a KM 9 na
Kazi ya kuweka kifusi imesimama kutokana
na mvua zinazoendelea kunyesha.
·
Matengenezo ya kawaida barabara ya
Kilolo - Ng'uruhe KM 7 na Kazi
inaendelea
·
Matengenezo ya kawaida barabara ya
Kitowo - Mwatasi KM 7.Kazi inaendelea.
Matengenezo ya sehemu korofi (Spot improvement)
jumla ya Km. 73 kwa mchanganuo
ufuatao:-
·
Matengenezo ya sehemu korofi barabara
ya Kidabaga - Bomalang'ombe 9 KM, Ilula - Vitono - Uhambingeto KM 7, Kilolo Mjini na Kazi inaendelea.
·
Matengenezo ya sehemu korofi barabara
ya Bomalang'ombe - Mwatasi KM 7, Ukumbi - Masege KM 5, Mawambala - Winome KM 6,
Wotalisoli - Udekwa KM 15, Mwatasi -Ng'ingula KM 6 , Msonza - Kimala KM 8. Kazi ya kuweka kifusi imesimama kutokana
na mvua zinazoendelea kunyesha
·
Matengenezo ya sehemu korofi barabara
ya Ikuvala - Kipaduka - Ikuka KM 11 na kazi imekamilika
Matengenezo
ya Muda maalum (Periodic Maintenace) barabara ya
Ilula - Ibumu KM 15 na barabara ya Makungu - Mlafu KM 6,
Aidha Wilaya inaendelea na ufunguzi wa
barabara mpya za Idete - Kiwalamo - Kimala
KM 16 na Kazi ya ujenzi wa barabara hizi umesimama kutokana na mvua
zinazoendelea kunyesha katika maeneo hayo. Pia ufunguzi wa Barabara ya Ihimbo –
Kitelewasi Km.20 unandelea kufanyika na Mkandarasi yupo eneo la kazi anaendelea
na ujenzi huo.
Madaraja/makalvati na mifereji ya maji
·
Ujenzi wa daraja barabara ya Ukumbi -
Pomerini (Concrete deck)kazi imekamilika
·
Ujenzi wa madaraja mawili na vivuko
barabara ya Idete - Kiwalamo – Kimala.kazi imesimama kutokana na mvua
zinazoendelea kunyesha.
·
Ujenzi wa Mifereji ya mawe barabara ya
Ilula - image ( Image no. 1),kazi inaendelea
·
Ujenzi wa Daraja la Kiwalamo 20m – 3
Span Kazi iko katika hatua ya manunuzi
Aidha Wilaya inaendelea na Ujenzi wa Nyumba 3 za watumishi Makao Makuu ya Wilaya na hatua
iliyofikia ni ya Manunuzi.
Matengenezo haya yanafanywa kwa kutumia fedha
zinazotokana na vyanzo mbalimbali baadhi ya vyanzo hivyo ni:-
- Fedha kutoka mfuko wa barabara (Road Fund)
- Fedha za Wadau/Wafadhili kutoka Food Aid Counter Part Fund (FACTF) na New Forest Co. LTD
- Fedha kutoka Ruzuku Maalum ya Maendeleo- Capital Development Grant (CDG)
SEKTA YA MAJI
Katika kipindi cha mwezi Januari 2013 hadi April 2013, Sekta ya Maji
imeendelea kutekekeleza shughuli mbalimbali za maendeleo ikiwa shughuli hizo
zinatarajia kutumia Jumla ya Tshs. Milioni mia saba na nne laki moja thelathini
na saba elfu (704,137,000/=) na tayari Tshs. Milion hamsini na nane laki mbili thelathini
na saba elfu( 58,237,000)
zimeshatumika.
Kwa mchanganuo ufuatao:-
·
Ujenzi wa mradi wa maji Ruahambuyuni ( hii ilikuwa
ahadi ya Mhe. Waziri Mkuu alipotembelea Ruaha Mbuyuni na Tayari Tshs. Milioni ishirini
(20,000,000/=) zimeshapokelewa). Kazi zilizopangwa ni pamoja
na kujenga chujio,kujenga pump Machine pamoja na survey.Aidha Upimaji (Survey)
ulifanyika kinachoendelea ni kazi ya usanifu
·
Ukarabati
wa mtego wa maji wa Idunduge unaopeleka maji katika kijiji cha Iyai- Image.
·
Usimamizi
wa uchimbaji visima vifupi na vya kati chini ya ufadhili wa MAUA projects
(Maji, Usafi na Afya) katika Vijiji vya Lundamatwe kisima 1 na Isoliwaya Visima
3.
·
Ujenzi wa mradi wa maji Kijiji cha Ikula na
Vitono ambao muda wowote utaanza kutekelezwa kwa kuwa Wakandarasi
wameshapatikana pamoja na idhini ya utekelezaji (no objection) toka Wizara ya
Maji/Benki ya Dunia.
·
Kuimarisha
mifumo ya maji katika Mamlaka za Maji katika Miji ya Ilula kwa upanuzi wa
mradi kwenda Mtua km.1.8,Madizini km2.3.Ukarabati
line kuu ya Ilomba,vifaa vya ujenzi vimeshanunuliwa na kazi inaendelea
kufanyika.
·
Kuimarisha
mifumo ya maji katika Mamlaka za Maji katika Miji ya Kilolo kwa Kupeleka maji Kitongoji cha
Itunduma km 2,kujenga vituo viwili vya maji,ujenzi wa tank lita 5000 pamoja na
ukarabati wa intake Na.2 ya maji (Mosongela).Kazi inaendelea kufanyika.
·
Aidha miradi ya maji ya Ruaha Mbuyuni na
Mamlaka za maji za Ilula na Kilolo zinaendelea kufanyika.
SEKTA YA
KILIMO,MIFUGO NA USHIRIKA
Katika kipindi hiki Sekta hii imefanya Shughuli mbalimbali zikiwemo
Kuwezesha uchanjaji wa mbwa dhidi ya kichaa cha mbwa,Kufanya mikutano ya
uhamasishaji kwa wakulima juu ya ufugaji wa ng’ombe wa maziwa katika vijiji vya Idegenda na
Mbawi,Kuwezesha uundaji wa vikundi viwili vya wafugaji wa ng’ombe wa
maziwa kwa vijiji vya Idegenda na Mbawi,Kutoa mafunzo kwa vikundi 2 vya Mbawi na Idegenda juu ya ufugaji bora wa
ng’ombe wa maziwa Kuandaa na kuweka mabango ya kuutambulisha mradi katika
vijiji hivyo na Kuwezesha
ununuzi na usambazaji wa mbuzi wa maziwa katika vijiji vya Kimala, Mhanga na
Idunda kwa Tshs.Milioni tisa, laki tano na ishirini na tatu elfu (9,523,000)
kwa ufadhili
wa Eastern Arc Mountains Conservation Endownment Fund (EAMCEF).
Kwa
upande wa Kitengo ya Ushirika ,shughuli
zilizofanyika ni pamoja na Kufanya ukaguzi wa hesabu za SACCOS za NYAIM (Nyanzwa,
Igunda na Mgowelo), Kilolo, Kitonga
na kikundi cha wakusanya nyanya Ilula.Kufanya uhamasishaji wa uundaji wa SACCOS
ya Image.Kutoa mafunzo ya usimamizi na uendeshaji wa SACCOS ya NYAIM kwa
viongozi wa bodi. Kufanya usajili wa SACCOS mpya ya Upendo iliyoanzishwa katika
kijiji cha Kitowo kata ya Ukumbi na SACCOS Mpya ya Mpoki ambayo makao makuu
yapo katika kata ya Ng’uruhe.
Aidha mpaka sasa tumepokea
kiasi cha Tshs.Milioni thelathini na nane
Laki tisa sabini na tano Mia saba thelathini na sita elfu (38,975,736/=) ikiwa ni kwa ajili ya vikundi katika vijiji vya Isele, Masisiwe,
Ng’ingula, Ng’ang’ange, Mdeke, Idasi, Mwatasi, Nyawegete na Luhindo kwa ajili
ya kuwezesha uanzishaji wa vitalu vya miche ya chai.
Bajeti ya mwaka 2012/2013 ni Tsh.Milioni mia tatu
sabini na tatu Laki nane tisini na moja elfu na thelathini na nne (373,891,034/=)
za Programu ya maendeleleo ya Kilimo Wilayani
District Agriculture Development Plans (DADPs).
SEKTA YA
ELIMU SEKONDARI
Katika kipindi cha Januari hadi Aprili Sekta ya
sekondari imeweza kutekeleza shughuli za maendeleo ikiwa ni pamoja na:-
·
Kugawa fedha za ruzuku
katika shule 22 za sekondari ambazo ni
Kilolo, Ilula, Dabaga, Kitowo, Lukani, Lulanzi, Lundamatwe, Madege, Masisiwe,
Mawambala, Mazombe, Mlafu, Mtitu, Ngangwe, Uhambingeto, Udizungwa, Lukosi,
Udekwa, Irole, Ukwega, Nyalumbu na Selebu.
·
Ujenzi wa madarasa mawili
katika shule mbili za lulanzi na Mawambala,
·
Ununuzi wa mobile laboratory
2 na kuzigawa katika shule mbili za kilolo
na kitowo,
·
Uendeshaji wa mtihani wa
kidato cha sita katika shule tatu za Pomerin, Image na Ilula.
·
Ukamilishaji wa ujenzi
wa madarasa 3 kwa kila shule za Sekondari za Madege,Mlafu,Mazombe,Mtitu,Lukosi
na Kitowo.
·
Ukamilishaji wa ujenzi wa
nyumba za walimu katika shule za sekondari za Ngangwe, Lundamatwe, Kilolo, Makwema
na Udekwa.
TAARIFA YA MFUKO WA ELIMU WA WILAYA (KETF)
·
Fedha zilizopo benki ni Tshs.
Milioni tano laki saba arobaini na mbili elfu mia
nane tisini na nane (5,742,898.00) kama
inavyoonesha kwenye bank statement.
·
Vifaa vilivyopo ni bati 270,
bati 30 ziligawiwa katika sekondari ya Makwema kuezekea choo cha shule,aidha
bati zilizobaki zitagawiwa katika shule za sekondari za Dabaga, Uhambingeto,
Ukwega
Jumla ya Tshs.Milioni
miamoja sitini na nane na thelathini na tisa elfu mia sita na moja (168,039,601) zimeingizwa
kwenye Akaunti za shule husika isipokuwa fedha za ruzuku.
USAJILI WA SHULE MPYA ZA SEKONDARI.
Usajili wa Shule mbili za
sekondari za Kata ambazo ni Shule ya
Sekondari ya Ipeta iliyopo Kata ya Bomalang’ombe imepewa namba ya usajili S.4688
na shule ya Sekondari ya Luganga iliyopo Kata ya Nyalumbu imepewa namba
ya Usajili ya S.4689.
Aidha shule ya Sekondari ya
Udzungwa imepewa kibali cha kuongeza mikondo ya Kidato cha tano kwa barua yenye
Kumb.Na.SPED/292/457/10/110 ya
tarehe 14/02/2013 iliyotolewa na
Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi.Masomo yatakayofundishwa ni ya Mchepuo wa CBG na HGL
kwa wasichana tu.
MAPOKEZI YA WALIMU WAPYA.
Katika kipindi cha Januari
hadi April 2013 Wilaya imepokea walimu wa shule za Msingi na Sekondari kwa
mchanganuo ufuatao:-
·
Wilaya imepokea walimu 150
wa Idara ya Elimu Msingi ambao tayari wamesharipoti na kufikishwa kwenye vituo
vya kazi.
·
Wilaya ilipangiwa walimu 82
wa shahada na walimu 42 wa stashahada.Walimu walioripoti na kupangiwa vituo vya
kazi ni walimu 66 wa shahada na walimu 40 wa stashahada. Hivyo walimu 18 bado
hawajaripoti.
SEKTA YA AFYA.
Sekta
ya Afya imetekeleza shughuli za Kununua dawa na vifaa tiba ili kuongezea pale
ambapo dawa toka MSD hazikutosha, Kufanya kikao cha pamoja na Waganga wafawidhi
wa vituo vya kutolea huduma, Maafisa Afya na CHMT (Council Health Management
Team). Kufanya usimamizi elekezi katika vituo 53 vya kutolea huduma za Afya
wilayani.Ununuzi wa Solar power na ufungaji Katika Zahanati ya Kimala. Ujenzi
wa shimo la kuchomea taka katika Kituo cha Afya Kidabaga( Placenta Pit).Kufanya
usambazaji wa chanjo, dawa na vifaa tiba pamoja na kulipa
gharama za mawasiliano (on call allowance) ikiwa jumla ya Tshs.Milioni
tisini laki tatu na thelathini na saba elfu
(90,337,000) zimetumika kukamilisha kazi hizo. Aidha fedha za Mfuko wa Pamoja wa Afya ( Health
Basket Fund), Mfuko wa Bima ya Afya ya
Jamii(CHF) na Matumizi mengineyo(OC) zimetumika kufanikisha
kazi hizi.
Aidha Wilaya inaendelea na Ujenzi
wa Hospitali ya Wilaya awamu ya pili na
kwa sasa ujenzi upo hatua ya
Msingi.Ujenzi wa Chumba cha upasuaji Kidabaga HC (Awamu ya pili) ikiwa kwa sasa
ipo hatua ya bimu,Ujenzi wa Zahanati mpya za Lugalo,Masege na Mbawi ikiwa kazi
hizi zipo hatua ya manunuzi kupitia Mpango wa maendeleo wa Afya ya Msingi (MMAM)
pamoja na fedha za Ruzuku Maalumu ya Maendeleo CDG(Capital Development Grant)
kwa kukamilisha ujenzi wa zahanati hizo.Ukarabati wa zahanati ya Ifuwa ambayo
imekamilika Jumla ya Tshs.Milioni miambili arobaini na tisa (249,000,000/=) zimetengwa kukamilisha kazi hizo.
SEKTA YA ARDHI,
MALIASILI, MISITU NA MAZINGIRA
Sekta ya Ardhi, Maliasili,Misitu na Mazingira imeweza Kupima mashamba ya wananchi katika
Kata ya Udekwa na Dabaga.Kutayarisha Database ya namba za nyumba kwa ajili
kukusanya kodi za majengo katika Mji wa Ilula.Kulipa fidia ya ardhi na mali kwa
wananchi waliotwaliwa ardhi zao kwa ajili ya uendelezaji wa Mji wa Kilolo
ambapo kiasi cha Tshs Milioni ishirini na tisa (29,000,000/=) zilitolewa fidia kwa wananchi 29.Kuandaa Mpango wa
Matumizi Bora ya Ardhi wa Kijiji kimoja
cha Ifuwa.Kutambulisha mradi wa upandaji miti, ufugaji nyuki na kilimo
cha uyoga katika vijiji 20 vya Nyanzwa, Mgowelo, Msosa, Mahenge, Irindi,
Magana, Ikokoto. Ilambo, Ibumu, Iyai, Image na 8, Isagwa, Makungu, Luhindo,
Lusinga, Ilamba, Ibofwe, Imalutwa, Mazombe na Lugalo.Kutoa mafunzo ya wajibu na
majukumu kwa kamati za maliasili na upimaji wa mipaka misitu kwa Vijiji vya
Masalali, Bomalangombe, Mkalanga, Nyanzwa na Mgowelo kwa jumla ya Tshs. Milioni sabini na nne laki nne
thelathini na sita elfu mia nne na kumi (74,436,410/=)
katika kukamilisha kazi hizo.
FEDHA ZA RUZUKU MAALUM YA MAENDELEO (CDG) KWENDA
NGAZI ZA VIJIJI
Katika kipindi cha Januari
hadi April, 2013, Miradi iliyowezeshwa kupitia fedha za Ruzuku Maalum ya
Maendeleo ni pamoja na:-
·
Ukamilishaji wa madarasa,vyoo na nyumba za walimu kwa shule
za Msingi 34
·
Ukamilishaji wa majengo kwa
sekondari za Ipeta,Ibumu,Ilula mwaya (Luganga sekondari),Ngagwe,Selebu,Irole,Kimala,Mhanga,Igunda,Dabaga
na Mawambala;
·
Ukamilishaji wa Wodi ya
Akina mama Ikula,Ukamilishaji wa zahanati ya Mbawi;
·
Ukamilishaji wa ofisi ya
Kijiji cha Lugalo,Itungi,Ng’ang’ange na
Ofisi ya kata Lugalo
Jumla ya Tshs.121, 000,000/= zimeingizwa kwenye
akaunti za Taasisi husika kama vijiji na shule na utekelezaji upo hatua
mbalimbali.
MFUKO
WA KUCHOCHEA MAENDELEO JIMBO LA KILOLO (CDCF)
Jumla ya Tshs 52,659,814/= zimepokelewa katika kipindi cha Januari hadi
April, 2013 kwa ajili ya kuendeleza shughuli mbalimbali za maendeleo katika
Jimbo la Kilolo ikiwemo kuchangia maeneo ambayo tayari wananchi wameshachangia
nguvu kazi.
·
Ukarabati/ukamilishaji wa ujenzi wa majengo kwa Shule za
Msingi 15 ambazo ni Luhindo, Luganga, Ikuvala, Mwaya, Uhambingeto, Iwungi,
Mtakuja, Ikokoto, Ibumu mkondo B, Isagwa, Wangama, Mdeke, Ndengisivili na
Masalali.
·
Kuwezesha ujenzi wa
mabweni Sekondari za Mlafu na Mawambala,
·
Kuwezesha Ujenzi wa Wodi la Akina mama zahanati ya Ikula,
·
Kufunga umeme wa jua (solar Power) zahanati ya Lukani
·
Ukamilishaji wa
ujenzi wa madarasa Sekondari za Ibumu na Ipeta.
Aidha Jumla ya Tshs.Milioni
ishirini na tatu na laki tano (23,500,000/=)
ziliidhinishwa na Kamati ya Mfuko wa Jimbo iliyokaa tarehe 05/03/2013 na
fedha ziliingizwa kwenye akaunti za Taasisi husika.Mgao wa awamu ya Pili
unatarajia kufanyika Mwanzoni mwa mwezi Mei, 2013.
Changamoto zilizojitokeza
katika kipindi cha Januari hadi April, 2013.
Wilaya ya Kilolo ilikabiliwa na changamoto
zifuatazo:
- Fedha zilizoidhinishwa kutofika kwa wakati au kufika pungufu.
- Bajeti ndogo hasa juu ya uboreshaji wa miundombinu ya barabara hali inayopelekea baadhi ya maeneo ya barabara za Idete – Itonya km 8, Msonza – Kimala km 7, Kimala – Idunda – Mhanga km 10, Mhanga – Itonya – Uluti km 16, Ng’ingula – Madege km 5, Ng’ingula – Masisiwe km 10, Kimala – Ukwega km 12, Makungu – Mlafu km 6, Ikokoto A – Ikokoto B km 6.5, Wotalisoli – Udekwa km18 na Ukumbi – Mawambala km 17 kutopitika hasa katika kipindi cha mvua.
iii.
Uchangiaji hafifu wa
Wananchi katika utekelezaji miradi ya maendeleo kama ambavyo maelekezo ya kisera yanavyosema,hali hii imepelekea
kuwa na ugumu na uchelewashaji katika utekelezaji wa miradi ya maendeleo.
iv.
Kutopata Watumishi wapya
(Ajira Mpya) walioko kwenye Mpango na bajeti 2011/12 isipokuwa walimu wa
Idaraya ya Elimu Msingi na Sekondari tu.
v.
Vikwazo juu ya ukusanyaji
wa mapato ya Halmashauri ya wilaya katika vipengele viwili kama ifuatavyo;
a)
Kutokuwepo kwa viwango vya leseni za biashara
toka Wizara ya TAMISEMI, Viwanda na Biashara.
b)
Ushuru utokanao na chanzo
cha Stendi ya Ilula, Magari kutoingia stendi na kulipa ushuru.
c)
Ukosefu wa fedha za
kulipia fidia za viwanja kwa wakati.
………………..
GERALD GUNINITA
MKUU WA WILAYA
KILOLO
0 comments:
Post a Comment