Kuna
watu ambao katika maisha yao ya kila siku hawana tabia ya kunywa maji mara kwa
mara .
Hii ni kutokana na kuona kero kwa kunywa maji kila wakati au kuona uvivu
wa kubeba chupa za maji au kulazimika kufuata mahali ambapo maji yanapatikana
lakini kubwa kuliko zote kati ya sababu hizo ni kutofahamu umuhimu wa kunywa
maji mara kwa mara katika maisha ya afya ya mwanadamu.
Maji ni sehemu muhimu ya maisha ya
mwanadamu na yana machango mkubwa sana katika afya ya mwili na kama yakinywewa
ipasavyo yanaweza kukuepusha na magonjwa mengi ambayo yatakufanya uishi maisha
marefu .
Maji yanakufanya uendelee kuonekana mdogo.
Maji yanafanya ngozi yako iwe na
vimeleo au mabaki muhimu ya maji muda wote na hivyo kuondoa adha ya ngozi
kuharibika kutokana na umri mkubwa . Maji kiasilia hurutubisha ngozi huku
ikijazia mistari ambayo huondoa makunyanzi na kuifanya ionekana kuwa nyororo na
laini.
Unywaji wa maji huondoa Msongo wa mawazo.
Unaweza ukashindwa kuamini jinsi
gani maji yana mchango kwenye afya ya saikolojia yako lakini ile sauti ya maji
yakiwa yanachuruzika inaweza kutuliza mawazo yako na kuondoa msongo wa mawazo .
Maji yasaidia kupunguza na kuponya mafua .
Unywaji wa maji husaidia kuondoa
mafua kwa wale wenye allergy ya vumbi na uchafu na pia kunawa mikono mara kwa
mara kwa maji masafi kunasaidia kuua vijidudu ambavyo huwafanya watu kupata
mafua mara kwa mara .
Maji yasaidia nywele.
Kwa wale wadau wa masuala ya urembo
hasa kina dada zaidi ya kuritubisha ngozi maji husaidia kung’arisha nywele .
Kuosha nywele kwa maji ambayo hayajachemshwa kwa kutumia virutubisho vya nywele
vya kutengeneza kama vile shampoo na mafuta maalum aina ya conditioner
yanazifanya nywele kuwa thabiti zaidi na kuondoa uwezekano wa kungoka hovyo
hovyo huku zikiwa na mn’gao .
Ngozi ya
mwili husaidiwa sana na maji.
Zaidi ya ngozi ya uso maji ni muhimu
kwa ngozi ya mwili kwa ujumla . Wakati wa kuoga maji ya moto au vugu vugu
hufanya ngozi ya mwili kuwa nyororo na yenye afya zaidi , maji husaidia kuondoa
ukavu ambao huondoa mvuto wa asili wa ngozi na kuipa afya kwa ujumla .
Maji husaidia kupunguza uzito wa mwili.
Kwa wale wenye matatizo ya uzito
ambayo wakati mwingine yanaweza yakawa hatari kwa afya yako kwa kusababisha
matatizo kama Presha ,kisukari na magonjwa ya moyo maji yanaweza kuwa kimbilio
lako. Kwa kujibu wa utafiti , watu wazima wanaokunywa glasi nane za maji kwa
siku yaani angalau glass mbili kwa kila baada ya saa kadhaa hasa kabla ya
wakati wa kula wanajikuta wakila chakula kidogo na hivyo kufanya mwili wako
kupata chakula kile kile kinachohitajika na mwili wako na hivyo kuondoa
uwezekano wa mwili wako kulimbikiza chakula kinachofanya uzito wako uendelee.
Maji huisaidia akili kufanya kazi vizuri .
Mwili unapokosa maji tatizo pekee
sio mtu kuhisi kiu wakati mwingine
ubongo huhisi kuchoka kirahisi na haraka pale ambapo mtu hajanywa maji muda
mrefu . Hisia kama hasira , uchovu wa akili , kuchanganyikiwa humtokea mtu
kirahisi wakati akiwa hajanywa maji muda mrefu na wakati mwingine hata kichwa
huuuma sana lakini suluhisho la yote haya ni kunywa maji mara kwa mara .
Muwasho wa koo.
Muwasho wa koo unaotokana na allergy
au mafua hutibiwa na maji , mtu anapopata tatizo hili suluhisho la haraka ni
kusukutua maji yenye chumvi lakini kuepsuah tatizo hili ni kuhakikisha koo
halikauki kwa muda mrefu .
Maji husaidia kupigana dhidi ya magonjwa .
Maji yana msaada mkubwa sana kwenye
kupambana na magonjwa mwilini mwako . Ni vizuri kunywa maji mara kwa mara
kuepusha mwili wako na magonjwa . Pia ulaji wa matunda husaidia kuupa mwili
maji muhimu yanayokuwa kinga dhidi ya magonjwa mbalimbali . Matunda kama
mapapai,matikiti maji,matango,machungwa ,ndizi,maembe yanauongezea mwili maji
ambayo yanakufanya ukae muda mrefu bila kuugua .
0 comments:
Post a Comment