Shirikisho
la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA) limetuma mapendekezo 10 ya
marekebisho ya Katiba yake kwa wanachama wake kwa njia ya waraka.
Mapendekezo
hayo yametumwa kwa kila nchi mwanachama kupitia waraka namba 1320,
ambapo wanachama kwa kupitia kwa mashirikisho yao ya mabara watapiga
kura ya ndiyo au hapa. Kwa upande wa Afrika, wanachama wa FIFA
wanatakiwa kuwasilisha kura zao kupitia Shirikisho la Mpira wa Miguu
Afrika (CAF).
Baadhi
ya mapendekezo hayo ni wajumbe wa Kamati ya Utendaji kuthibitishwa na
Mkutano Mkuu wa FIFA (FIFA Congress). Makamu wa Rais wa FIFA na wajumbe
wa Kamati ya Utendaji wanaochaguliwa katika mabara ambapo itabidi
wathibitishwe na FIFA Congress.
Muundo
wa Kamati ya Utendaji; nafasi moja ya vyama vya mpira wa miguu vya
Uingereza (British FAs) sasa inahamishiwa Shirikisho la Mpira wa Miguu
Ulaya (UEFA). Pia Mwenyekiti wa Kamati ya Ukaguzi ya FIFA anatakiwa
kushiriki vikao vya Kamati ya Utendaji bila kuwa na haki ya kupiga kura.
Uchaguzi
wa Rais; mgombea anatakiwa kuungwa mkono na idadi ya kutosha ya vyama
wanachama kutoka katika mabara mawili tofauti. Ukomo wa uongozi;
kuanzisha vipindi vya uongozi. Ukomo wa umri; ukomo wa umri usiozidi
miaka 72 wakati wa kugombea utekelezwe.
Uwakilishi
wa kutosha kwa makundi yenye maslahi katika FIFA; makundi yenye maslahi
katika mpira wa miguu kama wachezaji wapate uwakilishi katika Kamati ya
Mpira wa Miguu. Uteuzi wa mwenyeji wa Fainali za Kombe la Dunia; uteuzi
sasa ufanywe na Mkutano Mkuu wa TFF.
WATAZAMAJI 13,398 WAZISHUHUDIA YANGA, KAGERA
Watazamaji
13,398 wameshuhudia pambano la Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) kati ya Yanga
na Kagera Sugar lililochezwa juzi (Februari 27 mwaka huu) Uwanja wa
Taifa, Dar es Salaam na kuingiza sh. 77,117,000.
Mechi
hiyo namba 130 iliyochezeshwa na Simon Mberwa kutoka mkoani Pwani
ilimalizika kwa Yanga ambao wanaongoza VPL wakiwa na pointi 42 kuibuka
na ushindi wa bao 1-0 lililofungwa dakika ya 45 na Haruna Niyonzima.
Viingilio
vilikuwa sh. 5,000, sh. 8,000, sh. 15,000 na sh. 20,000 huku kila klabu
ikipata mgawo wa sh. 18,291,297.95 wakati Kodi ya Ongezeko la Thamani
(VAT) iliyolipwa ni sh. 11,763,610.17.
Kiingilio
cha sh. 5,000 ndicho kilichovutia watazamaji wengi ambapo waliokata
tiketi hizo walikuwa 11,908 na kuingiza sh. 59,540,000 wakati idadi
ndogo ya washabiki ilikuwa ya kiingilio cha sh. 20,000 kilichovutia
washabiki 80 na kuingiza sh. 1,600,000.
Mgawo
mwingine wa mapato hayo ni asilimia 15 ya uwanja sh. 9,300,659.97,
tiketi sh. 3,348,990, gharama za mechi sh. 5,580,395.98, Kamati ya Ligi
sh. 5,580,395.98, Mfuko wa Maendeleo ya Mpira wa Miguu (FDF) sh.
2,790,197.99 na Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Dar es Salaam (DRFA)
sh. 2,170,153.99.
POLISI KUIKABILI OLJORO KUNG’ANG’ANIA VPL
Polisi
Morogoro inaikaribisha Oljoro JKT ya Arusha kwenye Uwanja wa Jamhuri
mjini Morogoro katika mechi pekee ya Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) kuwania
ubingwa wa Tanzania Bara itakayochezwa kesho (Machi 2 mwaka huu).
Hata
hivyo, timu hizo haziko katika kinyang’anyiro cha kuwania ubingwa
ambapo Yanga ndiyo inayoongoza ligi hiyo ikiwa na pointi 42 wakati
Oljoro JKT inayofunzwa na Alex Mwamgaya ikiwa nazo 21 na Polisi Morogoro
pointi 15.
Oljoro
JKT iko katika nafasi ya tisa. Polisi Morogoro ambayo katika mzunguko
wa pili imebadilika ikiwa chini ya Kocha Adolf Rishard inashika nafasi
ya 12 ikiziacha mkiani Toto Africans yenye pointi 14 na African Lyon
ambayo ina pointi 13.
Ligi
hiyo itaendelea Jumatano (Machi 6 mwaka huu) kwa mechi kati ya Oljoro
JKT vs Tanzania Prisons (Sheikh Kaluta Amri Abeid), African Lyon vs Ruvu
Shooting (Azam Complex, Chamazi) na Mgambo Shooting vs Mtibwa Sugar
(Mkwakwani) wakati Machi 7 mwaka huu ni JKT Ruvu vs Kagera Sugar (Azam
Complex, Chamazi).
Machi
9 mwaka huu kutakuwa na mechi mbili; Yanga vs Toto Africans 9Uwanja wa
Taifa), na Azam vs Polisi Morogoro (Azam Complex, Chamazi).
VILLA SQUAD KUIVAA ASHANTI UNITED FDL
Michuano
ya Ligi Daraja la Kwanza (FDL) inaendelea kesho (Machi 2 mwaka huu)
katika makundi yote matatu. Villa Squad itaivaa Ashanti United kwenye
Uwanja wa Karume, Dar es Salaam katika moja ya mechi za kundi B.
Kundi
A ni mechi kati ya Kurugenzi ya Mafinga dhidi ya Mbeya City wakati
Polisi Iringa vs JKT Mlale, na Majimaji vs Mkamba Rangers zilizokuwa
zicheze kesho (Machi 2 mwaka huu), sasa zitaumana Machi 3 mwaka huu
mjini Iringa na mjini Songea.
Pia
kundi B kesho (Machi 2 mwaka huu) ni Green Warriors vs Transit Camp
(Mlandizi) wakati keshokutwa (Machi 3 mwaka huu) Polisi Dar vs Tessema
(Karume) na Ndanda vs Moro United katika Uwanja wa Nangwanda Sijaona
mjini Mtwara.
Mechi
za kundi C kesho ni JKT Kanembwa vs Polisi Tabora (Lake Tanganyika),
Polisi Mara vs Polisi Dodoma (Karume, Musoma), Morani vs Pamba (Kiteto)
na Mwadui vs Rhino Rangers (Kambarage, Shinyanga).
Boniface Wambura
Ofisa Habari
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)
0 comments:
Post a Comment