Wakazi
wa Wilaya ya Ileje wanaoishi mikoa ya Iringa,Njombe,Rukwa na Mbeya Mjini,kwa
pamoja wamemuomba Raisi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,kuona umuhimu wa
kubadilisha mapendekezo ya Kamati ya Ushauri ya Mkoa wa Mbeya iliyopendekeza makao
makuu ya mkoa mpya wa Songwe yawe eneo la Mkwajuni wilayani Chunya,kwa madai
kuwa ni mbali ukilinganisha na Jiografia ya wilaya ya ileje.
Wananchi
wa wilaya ya Ileje wametoa maombi yao wakati wa Kongamano lililoshirikisha
wakazi wa ileje wanaoishi Nje ya wilaya hiyo,lililofanyika katika ukumbi wa
Kiwira Motel Jijini Mbeya,wakijadiliana maendeleo ya wilaya hiyo pamoja
na mgawanyo wa mkoa wa Mbeya na kupata mkoa mwingine mpya,ambao wameomba
mapendekezo ya makao makuu ya mkoa huo yasogezwe.
Mbunge
wa Jimbo la Ileje Aliko Kibona ambaye pia alikuwepo katika Mkutano huo
alisema kwa niaba ya Wananchi wa Ileje hayuko tayari kukubaliana na
maamuzi ya Kupeleka Makao makuu Mkwajuni Wilayani Chunya.na kuongeza kuwa chama cha mapinduzi kitakua katika wakati mgumu km maamuzi hayo hayatabadilishwa,
Wakizungumza
katika Mkutano huo Wananchi hao wamedai kuwa umbali kutoka Wilayani Ileje
kwenda Mbeya Mjini ni mbali sana hivyo kuwapeleka Mkwajuni ni kuzidi
kuwaongezea safari zaidi.
Yohana
Seme Mkazi wa Ileje amesema lengo la kugawanya Mkoa ni kusogeza huduma
kwa Wananchi lakini Mapendekezo ya Kupeleka Makao makuu ya Mkoa Wilayani Chunya
ni kupokonya huduma kwa Wakazi wa Ileje ambao huduma nyingi hutegemea Nchi
jirani ya Malawi.
Mjadala
wao wanaileje ukaenda mbali zaidi,baada ya mapendekezo ya awali ya wajumbe wa
kamati ya ushauri ya Mkoa wa Mbeya,kupendekeza makao makuu ya mkoa wa Songwe
yawe ni Mkwajuni Kilometa 321 kutoka kusini mwa wilaya ya Ileje.
Kutokana
na umuhimu wa Kongamano hili,Mbunge wa Jimbo la Ileje Aliko Kibona ambaye
pia alikuwepo katika Mkutano huo alisema kwa niaba ya Wananchi wa Ileje hayuko
tayari kukubaliana na maamuzi ya Kupeleka Makao makuu Mkwajuni Wilayani Chunya.
Kibona
amesema mapendekezo ya Wanaileje ni kwamba Makao makuu ya Mkoa wa Songwe
yasogezwe na kuwekwa katika kijiji cha Henje wilayani Mbozi, mapendekezo ambayo
yameungwa Mkono na Wakazi wa Momba, Mbozi na Ileje yenyewe.
Na Mbeya yetu
0 comments:
Post a Comment