Katibu Mkuu wa Shirikisho la Mpira wa Miguu
nchini (TFF), Mwesigwa Selestine ametuma salamu za rambi rambi kwa famili
aliyewahi kuwa Katibu Mkuu wa TFF, Fredrick Mwakalebela kufuatia kufiwa na baba
yake mzazi jana mjini Irinnga na mazishi yakitarajiwa kufanyika kesho mjini
Iringa.
Aidha TFF imetuma salam za rambi rambi kwa kocha mkuu wa
timu ya Mbeya City, Juma Mwambusi kufutia kufiwa na mama yake mzazi mjini
Mbeya.
TFF pia imetuma salam za rambi rambi kwa familia ya
mtangazi maarufu wa wa michezo nchini Ezekiel Malongo aliyefariki dunia
jana.
Katika salam zake kwa familia ya Mwakalebela, Mwambusi na
Malongo, Mwesigwa amesema wanawapa sana pole wafiwa kwa kuondokewa na wapendwa
wao na kusema kwa niaba ya TFF, familia ya mpira na watanzania wote wapo nao
pamoja katika kipindi hichi cha maombolezo.
0 comments:
Post a Comment