Timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars)
inayodhaminiwa na bia ya Kilimanjaro Premium Lager inaondoka nchini leo jioni
kuelekea Kampala - Uganda kwa ajili ya mchezo wake wa marudiano dhidi ya The
Cranes siku ya jumamosi.
Kikosi cha Taifa Stars kinaondoka kikiwa na wachezaji 20,
bechi la ufundi 7, pamoja na viongozi kwa shirika la ndege la Rwanda (Rwada
Airi) ambapo wanatarajiwa kuwasili uwanja wa Entebe majira ya saa 3 usiku kwa
saa za Afrika Mashariki na Kati.
Mchezo wa jumamosi ni wa marudiano kuwania kufuzu kwa
fainali za Afrika kwa wachezaji wa ndani (CHAN) zitakazofanyika nchini Rwanda,
huku mechi hiyo ikichezwa saa 10 jioni katika uwanja wa Nakivubo.
Kocha mkuu wa Taifa Stars, Charles Mkwasa amesema vijana
wake wamefanya mazoezi vizuri katika kipindi chote cha maandalizi, na sasa wako
tayari kwa mchezo huo, mipango ikiwa ni kupata ushindi siku ya jumamosi.
Aidha Mkwasa amesema watawakosa wachezaji wawili, Abdi
Banda na Mohamed Hussein (Tshabalala) waliopata majeruhi jana wakati wa mazoezi
yaliyofanyika uwanja wa Boko Vatereani, na kusema nafasi zao zitazibwa na
wachezaji waliopo kambini.
Wachezaji wanaosafiri ni: Ally Mustafa, Mudathir Khamis,
Juma Abdul, Shomari Kapombe, Haji Mngwali, Michael Aidani, Hassan Isihaka, Kelvin
Yondani, Nadir Haroub, Frank Domayo, Mudathir Yahya, Salum Telela, Said Ndemla,
Saimon Msuva, Deus Kaseke, Ramadhan Singano, Atupele Green, Rashid Mandawa,
John Bocco na Ame Ally.
0 comments:
Post a Comment