Hatimaye
Kikosi kazi cha Shirikisho la soka Duniani FIFA kilichopewa jukumu la
kuchunguza ni muda gani mzuri wa kufanyika kwa fainali za kombe la dunia nchini
Qatar mwaka 2022 kimemaliza kazi yake.
Kikosi hicho
kinachoongozwa na Sheikh Salman bin Ebrahim Al-Khalifa
kimependekeza fainali za kombe la dunia nchini Qatar zifanyike kuanzia mwezi wa kumi
na moja na mwezi wa kumi na mbili.
Taarifa
zaidi za kikosi kazi hicho zimesema kuwa kipindi cha miezi ya Novemba na
Decemba joto hupungua toka nyuzi joto 40 mpaka nyuzi joto 20 mpaka 29.
Taarifa
hii imeonekana kupingwa na watu mbalimbali hasa klabu za Ulaya ambazo zinahofia
ratiba hiyo ya kombe la dunia inaweza kuingiliana na ratiba ya Ligi za Ulaya.
Mchezaji
wa zamani wa timu ya Taifa ya England Trevor Sinclair anaenda mbali zaidi kwa
kusema kuwa nchi zilizoshindana na Qatar
kuomba kuandaa fainali za kombe la dunia mwaka 2022 ambazo ni Australia, Japan,
Korea Kusini na Marekani zipewe uenyeji wa fainali za kombe la dunia kwa mwaka huo.
Mchakato
wa kumtafuta mwenyeji wa fainali za kombe la dunia umekuwa na malalamiko mengi
sana kwani mchakato huo umehusishwa na
rushwa kwa Shirikisho la soka duniani FIFA ambapo Mwaka jana Rais wa FIFA Sepp
Blatter aliunda kamati ya kuchunguza mchakato huo kamati iliyoongozwa na
mwanasheria Michael Garcia.
Hata hivyo
Ripoti ya Garcia ilionesha kuwa mchakato wa kumpata mwenyeji wa fainali za
mwaka 2022 ulikuwa na dosari ripoti ambayo ilipingwa na FIFA wenyewe.
0 comments:
Post a Comment