Kumekuwa na maandamano ya dakika za mwisho mwisho mjini Paris, siku
mbili kabla ya bunge la Ufaransa kuidhinisha sheria inayohalalisha ndoa za
jinsia moja.
Wanaopinga sheria hiyo walikusanyika katika eneo la
Montparnasse la mji mkuu katika juhudi za mwisho mwisho za kuizuia sheria
hiyo.
Maandamano mengine ya kundi hasimu pia yaliandaliwa jana kuiunga
mkono sheria hiyo.
Zaidi ya watu 100 wamekamatwa katika kipindi cha wiki
moja iliyopita katika maandamano mengine ya kupinga ndoa za jinsia moja.
Makundi ya kutetea haki za binadamu pia yameripoti ongezeko la matusi na
mashambulizi ya kimwili dhidi ya jamii ya mashoga na wasagaji nchini
Ufaransa.
Ufaransa inatarajiwa kuwa nchi ya 14 kuhalalisha ndoa za jinsia
moja, kufuatia kuidhinishwa sheria hiyo nchini New Zealand wiki iliyopita.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment