Main Menu

Wednesday, June 26, 2013

BARAZA LA VYAMA VYA SIASA LADAI KUWA NA MWARUBAINI WA MACHAFUKO NCHINI


Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Anne Makinda (kulia) amekutana na Baraza la Vyama vya Siasa nchini chini ya Mwenyekiti wake Bwana Peter Mziray (kushoto) na kumweleza kuwa Baraza hili linao mwarobaini wa kumaliza machafuko yanayojitokeza nchini kwa sasa.

 Aidha wajumbe wa Baraza hilo wamemwomba Spika ili wakutane na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete ili waweza kutoa ushauri wao kuhusu machafuko yanayotokea Mtwara, Arusha na kwingineko nchini na jinsi ya kukabiliana nayo.
Wajumbe wa Baraza la Vyama vya Siasa nchini chini wakishiriki mkutano huo.

Picha na Prosper Minja - Bunge


0 comments:

Post a Comment