NYOTA Cristiano Ronaldo amerejea
Manchester na kuifungia bao la ushindi Real Madrid lililoitoa timu yake
ya zamani katika Ligi ya Mabingwa Ulaya usiku huu Uwanja wa Old
Trafford.
Sir Alex Ferguson alimuanzishia benchi
Wayne Rooney, lakini wenyeji ndio waliokuwa wa kwanza kupata bao mapema
kipindi cha pili, baada ya Sergio Ramos kujifunga.
Lakini mambo yaliwaharibikia baadaye
kidogo tu Man United, baada ya Luis Nani kuonyeshwa kadi nyekundu ya
moja kwa moja kwa kumchezea rafu Alvaro Arbeloa.
Na baada ya hapo, bao la Luka Modric
lilifuatiwa na bao la Ronaldo dakika tatu baadaye, hivyo vigogo hao wa
Hispania kutinga Robo Fainali.
hapa ronaldo sijui alikua anawaomba msamaha mashabiki wa man u
Kiungo wa zamani wa Spurs, Modric akifunga bao la kusawazisha
ronaldo akiwaua ndg zake
Beki wa Real akijifunga
Kadi nyekundu: Hapa ndipo ilipofia United baada ya kupungukiwa mchezaji mmoja
Akitokea benchi: Rooney akipasha kutokea benchi
Welbeck alikaribia kufunga leo, lakini alikuwa ameotea
Vidic alipiga kichwa kikagonga mwamba kipindi cha kwanza
Giggs amecheza mechi ya 1,000 leo Man United
Ronaldo amepata mapokezi mazuri leo Old Trafford
Ronaldo alikuwa katika wakati mzuri leoOld Trafford
Ronaldo akipasua Old Trafford
0 comments:
Post a Comment