Rais wa Venezuela, Hugo Chavez,
amefariki dunia baada ya kuugua kwa miaka miwili ugonjwa wa saratani na hivyo
kufikisha ukingoni uongozi wake wa miaka kumi na nne katika taifa hilo la
Amerika ya kusini lenye utajiri mkubwa wa mafuta.
Makamu wa Rais wa Venezuela, Nicolas
Maduro, ametangaza kupitia kituo cha televisheni nchini humo kuwa Chavez mwenye
umri wa miaka 58 ameaga dunia na kusema kifo chake kimewaacha na uchungu
mwingi.
Chavez amefariki katika hospitali ya
kijeshi huko Caracass baada ya kuugua kwa muda na kufanyiwa upasuaji mara
nne uliosababisha afya yake kuzorota.
Serikali ya Venezuela imetangaza
siku saba za maombolezo ya kitaifa na kwamba Rais huyo atazikwa Ijumaa hii.
Mwezi Oktoba mwaka jana Chavez
alishinda uchaguzi lakini hali yake ya afya ilizorota kiasi cha kutoapishwa.
0 comments:
Post a Comment