Wednesday, March 6, 2013
WAKENYA WAENDELEA KUSUBIRI MSHINDI WA UCHAGUZI WA RAIS
mkuu wa tume ya uchaguzi nchini kenya
Tume ya uchaguzi nchini Kenya hii leo inataraji kutangaza matokeo ya mwisho ya kura za urais, baada ya matokeo ya mwanzo kumwonyesha mgombea wa muungano wa Jubilee, Uhuru Kenyatta, akiongoza.
Shughuli ya kuhesabu kura tangu uchaguzi huo wa Jumatatu inaendelea polepole, na mfumo mpya wa elektroniki wa kupiga kura umekumbwa na hitilafu, hali inayosababisha malalamiko kutoka kwa vyama vya kisiasa na pia wasiwasi miongoni mwa wapiga kura kwamba zoezi hilo lililokikumbwa na udanganyifu, linaweza kusababisha machafuko mengine kama ya mwaka wa 2007.
Naibu Waziri Mkuu Uhuru Kenyatta mwenye umri wa miaka 51, amekuwa akiongoza katika matokeo ya mwanzo tangu kura zilipoanza kuhesabiwa, lakini baadhi ya maeneo ambayo ni ngome za mpinzani wake Waziri Mkuu, Raila Odinga, mwenye umri wa miaka 68, bado hayajatangaza matokeo.
Tume ya uchaguzi imesema itatumia matokeo yatakayowasilishwa leo usiku kwenye makaratasi katika kituo kikuu cha hesabu jijini Nairobi.
Imewataka wakenya kuwa watulivu wakati wakisubiri matokeo hayo leo.
Mpaka sasa Kenyatta yupo mbele kwa asilimia 53 dhidi ya Odinga na asilimia 42.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment