Wanaharakati wa
haki za binaadamu katika pembe mbalimbali za dunia wameendelea kuunga mkono
mgomo wa chakula wa wafungwa wa jela ya Guantanamo.
Kwa mujibu wa
ripoti iliyotangazwa na televisheni ya PRESS TV, mgomo wa wanaharakati hao wa
haki za binaadamu katika pembe mbalimbali za dunia unafanyika kama ishara ya
kuungana na wafungwa hao wanaoendelea kuzuiliwa katika jela ya kutisha ya
Guantanamo.
Mgomo huo
ulianza tarehe 24 Machi na unatarajia kuendelea hadi tarehe 30 ya mwezi huu.
Mbali na mgomo
huo, wanaharakati hao wamepanga kufanya mikusanyiko kadhaa katika nchi kadhaa
katika kuwaunga mkono wafungwa hao.
Tarehe 14 mwezi
huu mawakili 45 wanaowatetea baadhi ya wafungwa wanaoshikiliwa katika jela hiyo
ya Guantanamo walimtumia barua ya wazi Waziri wa Ulinzi wa Marekani Chuck Hagel
wakimtaarifu kuhusu suala hilo na kumtaka achukue hatua za haraka ili kumaliza
mgomo huo.
Wafungwa hao
walianza mgomo huo tangu Februari 6 mwaka huu baada ya wafanyakazi wa jela hiyo
ya Guantanamo kupora vitu vya wafungwa hao zikiwemo barua, picha na kuzivunjia
heshima nakala za kitabu kitukufu cha Qu'rani wakati walipozikagua selo zao.
0 comments:
Post a Comment