Shirikisho
la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) na kampuni ya Azam Media leo (Agosti
30 mwaka huu) wamesaini mkataba wa haki za kipekee za televisheni
(exclusive rights) utakaoiwezesha Azam TV kuonesha mechi za Ligi Kuu ya
Vodacom (VPL).
Mkataba
huo wa miaka mitatu wenye thamani y ash. 5,560,800,000 umesainiwa
kwenye hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam. Makamu wa Rais, Athuman
Nyamlani amesaini kwa niaba ya TFF wakati aliyesaini kwa upande wa Azam
Media ni Ofisa Mtendaji Mkuu wa kampuni hiyo Thys Torrington.
Ligi
Kuu ya Tanzania sasa itakuwa ikipatikana kupitia kisimbuzi (decorder)
cha Azam TV kitakachokuwa na chaneli zaidi ya 50. Mechi hizo
zinatarajiwa kuoneshwa moja kwa moja wakati wowote kuanzia mwezi ujao.
Makamu
wa Rais wa TFF, Nyamlani amesema udhamini huo wa televisheni ni fursa
pana kwa klabu kwani zitaweza kujitangaza zaidi huku wachezaji nao
wakipata soko zaidi za mpira wa miguu.
KOCHA KIM AONGEZA MMOJA TAIFA STARS
Kocha
Mkuu wa Taifa Stars, Kim Poulsen ameongeza kwenye kikosi chake beki
David Mwantika kwa ajili ya mechi ya Kombe la Dunia dhidi ya Gambia
itakayochezwa Septemba 7 mwaka huu jijini Banjul.
Mwantika
ameitwa kwenye kikosi hicho kuziba nafasi ya beki Kelvin Yondani ambaye
ni majeruhi. Wachezaji ambao ni majeruhi na Kim amewaondoa kwenye
kikosi hicho ni waweze kushughulikia matibabu yao ni Athuman Idd,
Shomari Kapombe na John Bocco.
Taifa
Stars imeingia kambini jana (Agosti 29 mwaka huu) na imeanza mazoezi
leo jioni kwenye Uwanja wa Kumbukumbu ya Karume. Timu hiyo
inayodhaminiwa na Kilimanjaro Premium Lager pia itakuwa ikifanya mazoezi
kwenye Uwanja wa Taifa.
Boniface Wambura
Ofisa Habari
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)
0 comments:
Post a Comment