Uhuru Kenyatta ndiye Rais wa nne wa
Jamuhuri ya Kenya baada ya tume ya uchaguzi kumtangaza kushinda uchaguzi wa
kihistoria wa Kenya.
Ni baada ya siku tano tangu wakenya
kupiga kura kuwachagua rais, magavana, maseneta , waakilishi wa bunge,
waakislihi wanawake na waakilishi wa wodi.
Uhuru alipata zaidi ya asilimia
hamsini ya kura zilizohitajika ili kupata ushindi kulingana na mahitaji ya
katiba mpya ya nchi.
Matokeo hayo yalionyesha kuwa Uhuru
Kenyatta ameshinda na hivyo kuepuka duru ya pili ya uchaguzi.
Takwimu kutoka tume ya uchaguzi
zinasema Kenyatta ameshinda asilimia hamsini nukta tatu za kura zote
zilizopigwa.
Tume ya uchaguzi ilichukua zaidi ya
masaa matano kukagua hesabu ya kura hizo kabla ya kutangaza matokeo hii leo
siku tano baada yawakenya kupiga kura.
Matokeo yaliyotolewa na tume ya
uchaguzi yanaonyesha kuwa Uhuru alipata kura 6,173,433 huku mpinzani wake Raila
Odinga akipata 5,340,546
Kenyatta anakabiliwa na mashtaka
katika mahakama ya kimataifa ya ICC kuhusiana na ghasia za baada ya uchaguzi
mkuu wa mwaka wa 2007.
Awali duru zilisema iwapo Kenyatta
atakabidhiwa ushindi katika raundi ya kwanza, mpinzani wake waziri Mkuu Raila
Odinga atakwenda mahakamani kupinga matokeo hayo.
Tume hiyo pia imemtangaza mshindi wa
uchaguzi huo kwa kuwa ametimiza masharti ya kikatiba ya kutangazwa kuwa rais wa
nne wa Kenya..
Vile vile mgombea huyo pia lazima
awe ameshinda asilimia 25% katika nusu ya County zote 47 nchini kenya.
Mwenyekiti wa Tume huru ya Uchaguzi na mipaka Isaka Hassan
amemtangaza Uhuru Kenyatta kuwa rais mpya wa Kenya.
Awali Waziri Mkuu Raila Odinga
alikuwa amewaalika waandishi wa habari nyumbani kwake kwa mkutano maalum ili
azungumzie maswala ya matokeo ya urais lakini baadaye mkutano huo uliakhirishwa,
baada ya tume ya uchaguzi kutoa tangazo lake la mwisho.
Raila Odinga wa muungano wa CORD, ameelezea malalamishi kuhusu
matokeo ya uchaguzi wa urais yaliyompa ushindi Uhuru Kenyatta.
Odinga amesema kuwa udanganyifu ulitokea katika shughuli ya
kuhesabu kura kwa kutumia mfumo wa zamani baada ya mitambo ya elektroniki
kugoma hali iliyohujumu demokrasia.
Mseamaji wa Raila Odinga, Anyang'
Nyong'o asema kuwa muungano wa CORD ulipinga matokeo ya mwisho ya uchaguzi
wa urais na kuitaka tume ya uchaguzi kutoyatangaza lakini walipuuzwa.
0 comments:
Post a Comment