Tume hiyo inapendekeza kwamba Rais ashirikiane na
mihimili mingine ya dola katika uteuzi huo, huku ikiwataja Mawaziri na
Naibu Mawaziri, Jaji Mkuu, Naibu Jaji Mkuu na Katibu Mkuu Kiongozi kuwa
uteuzi wao utakapofanywa na Rais lazima uthibitishwe na Bunge.
Mapendekezo hayo ni tofauti na hali ilivyo sasa
wakati uteuzi unaofanywa na Rais hauthibitishwi na Bunge, isipokuwa
nafasi ya Waziri Mkuu na Makamu wa Rais itapotokea ikawa wazi kwa sababu
zozote zile.
Pia, tume inapendekeza Rais ashauriane na chombo
kipya kitakachoundwa cha Baraza la Ulinzi la Taifa kuwateua viongozi
wote wa taasisi za ulinzi nchini.
Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Jaji
Joseph Warioba alisema mfumo wa utawala utaendelea kuwa kama ulivyo hivi
sasa na kwamba, Rais ndiye mtendaji wa Jamhuri ya Muungano na
atachaguliwa moja kwa moja na wananchi.
Jaji Warioba alisema Tume imependekeza mgombea
urais lazima apate zaidi ya asilimia 50 ya kura zilizopigwa na kwamba,
kinga ya kutokuhoji matokeo ya uchaguzi mahakamani iondolewe.
“Mgombea urais anaweza kupendekezwa na chama cha
siasa au kuwa mgombea huru, mgombea wa nafasi hiyo atatangazwa kuwa
mshindi iwapo atakuwa amepata zaidi ya asilimia 50 ya kura zote
zilizopigwa,” alisema Jaji Warioba na kuongeza: “Hata hivyo, matokeo ya
uchaguzi wa Rais yanaweza kulalamikiwa mahakamani, lakini siyo kila mtu
anaweza kufungua kesi, wanaoweza kufungua kesi ni wagombea urais na
Mahakama ya Juu pekee ndiyo itakuwa na mamlaka na uwezo wa kusikiliza
malalamiko kuhusu matokeo ya uchaguzi wa Rais na shauri lazima liamuliwe
ndani ya mwezi mmoja, yaani siku 30.”
Alisema Tume inapendekeza Rais achaguliwe moja kwa moja na wananchi na kwamba, suala la umri pia lilijadiliwa kwa upana.
“Wengine walisema umri wa mtu kuruhusiwa kugombea
urais uwe miaka 35 au 50 na kuendelea, Tume imeyachambua maoni yote na
ikafanya utafiti kwa kupitia Katiba za nchi zingine ,” alisema Jaji
Warioba na kuongeza:
“Wengi walioomba kugombea nafasi hiyo walikuwa na
umri wa miaka 40 au zaidi, kwa kuzingatia maoni ya wananchi, utafiti na
hali halisi, Tume imependekeza Rais aendelee kuchaguliwa na wananchi
pamoja na sifa nyingine mtu atakayegombea Urais asiwe chini ya miaka
40.”
Kutokupunguzwa kwa umri wa urais kutakuwa ni pigo
kwa wansiasa vijana nchini waliopendekeza ushushwe na kuwa miaka 35,
akiwamo Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe na Naibu Waziri wa
Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, Januari Makamba.
Zitto, Makamba watoa kauli.
Tume ya Mabadiliko ya Katiba imependekeza katika rasimu ya
Katiba Mpya ukomo wa wabunge na kufutwa kwa nafasi za Viti Maalumu
bungeni.
Akizungumzia suala hilo jana, Zitto alisema uamuzi huo wa umri
hana la kusema, kwa sababu yaliyotolewa ni mapendekezo ya Tume na
kwamba, Chadema watatoa kauli baada ya viongozi kuwasiliana.
Kwa upande wake, Makamba iwapo amebadili msimamo wake, alisema: “Suala la umri siyo kigezo pekee cha kupata uongozi mzuri.”
Makamba alisema ujana wala uzee siyo kigezo cha kumnyima mtu uongozi.
Siku za nyuma Makamba, ambaye ni Mbunge wa
Bumbuli, aliwahi kunukuliwa akitaka umri wa kugombea urais uwe miaka 35
badala ya 40 ya sasa.
Alisema suala la umri lisingemwathiri binafsi, kwani mwaka 2015 atakuwa na umri wa miaka 41.
“Ninapongeza Watanzania kwa kutoa maoni yao na kutaka vijana kupewa nafasi za uongozi,” aliongeza Makamba.
VITI MAALUM VYAPIGWA CHINI
VITI MAALUM VYAPIGWA CHINI
Mwenyekiti wa tume hiyo, Jaji Mstaafu Joseph
Warioba alisema jana, wanapendekeza kwamba ubunge uwe na ukomo wa
vipindi vitatu vya miaka mitano, mitano akimaanisha kwamba kipindi cha
mtu kuwa mbunge hakiwezi kuvuka miaka 15.
Rasimu hiyo ya Katiba imependekeza kutokuwapo tena
kwa Viti Maalumu na badala yake, imetaka kuwapo kwa nafasi tano za
uteuzi zibaki kwa Rais ambazo zitahusisha makundi maalumu ya watu wenye
ulemavu pekee.
Jaji Warioba alisema Tume imependekeza kuwapo kwa
majimbo 25 ya uchaguzi kwa Tanzania Bara na 20 kwa Zanzibar ambayo kila
moja litakuwa na wabunge wawili, mwanamke na mwanamume.
Kwa mujibu wa rasimu hiyo, majimbo hayo ni mikoa 25 ya Tanzania Bara na wilaya 10 za Zanzibar. Kwa maana hiyo, Bunge la Muungano litakuwa dogo lenye wabunge 75.
Kwa mujibu wa rasimu hiyo, majimbo hayo ni mikoa 25 ya Tanzania Bara na wilaya 10 za Zanzibar. Kwa maana hiyo, Bunge la Muungano litakuwa dogo lenye wabunge 75.
Mwenyekiti huyo alisema, wananchi watakuwa na
mamlaka ya kumwondoa madarakani mbunge wao endapo hawataridhishwa na
utendaji kazi wake.
Alisema hakutakuwa na uchaguzi mdogo wa wabunge
kwa wabunge watakaopitia kwenye vyama vya siasa na badala yake jimbo
litakapokuwa wazi chama kilichokuwa kikiongoza kitateua atakayeshika
wadhifa huo.
“Uchaguzi mdogo utafanyika pindi tu aliyekuwa
akiongoza alitokana na mgombea huru (binafsi) hivyo, Tume huru ya
Uchaguzi itatakiwa kuandaa uchaguzi mdogo,” alisema Jaji Warioba.
Kuhusu kiti cha Spika na Naibu Spika, alisema
baada ya kupokea maoni na wananchi mbalimbali, Tume hiyo imependekeza
viongozi hao wasitokane na vyama vya siasa.
Alisema Tume inapendekeza Spika na Naibu Spika wasitokane na wabunge na wasiwe viongozi wa vyama vya siasa wala wasitokane na asasi za kiraia ambao wataidhinishwa na Bunge.
Alisema Tume inapendekeza Spika na Naibu Spika wasitokane na wabunge na wasiwe viongozi wa vyama vya siasa wala wasitokane na asasi za kiraia ambao wataidhinishwa na Bunge.
WANANCHI WAFURAHIA MAPENDEKEZO
Mkazi wa Uhindini, Mbeya, Boniface Mwakinga
alisema amefurahishwa na mapendekezo yanayotaka kuwapo kwa ukomo wa
madaraka ya wabunge.
Mfanyakazi wa Hospitali ya Kilema, Kilimanjaro,
Dennis Mfumbulwa alisema kati ya mambo yaliyomgusa katika rasimu hiyo ni
hatua ya wananchi kupewa nguvu ya kumwondoa mbunge ambaye hawajibiki
kwa wapigakura wake akisema hilo sasa ni kitanzi kwa wabunge
wababaishaji.
Mbunge wa Bunge la Afrika ya Mashariki, Shyrose
Bhanji alieleza kufurahishwa kwake na kuondolewa kwa Viti Maalumu na
kupendekezwa kwa utaratibu mpya wa kusimama na kugombea wanawake
majimboni.
“Lengo la kuanzishwa Viti Maalum ilikuwa ni kuwapa upendeleo maalumu wanawake kuingia katika siasa na vyombo vya uamuzi, nadhani imefanikiwa na sasa tunapaswa kushindanishwa sisi kwa sisi,” alisema Bhanji.
mwananchi.
“Lengo la kuanzishwa Viti Maalum ilikuwa ni kuwapa upendeleo maalumu wanawake kuingia katika siasa na vyombo vya uamuzi, nadhani imefanikiwa na sasa tunapaswa kushindanishwa sisi kwa sisi,” alisema Bhanji.
mwananchi.
0 comments:
Post a Comment