Inspekta Jenerali wa Polisi, IGP Said Mwema, amefanya mabadiliko ya makamanda na wakuu wa upelelezi katika baadhi ya mikoa hapa nchini.
Katika mabadiliko hayo aliyekuwa Kamanda wa Polisi mkoa wa Iringa, Naibu Kamishna wa Polisi (DCP) Michael Kamhanda amehamishiwa Makao Makuu ya Polisi na nafasi yake inachukuliwa na Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP) Ramadhani Mungi ambae alikuwa Makao Makuu ya Upelelezi wa Makosa ya Jinai.
Aidha, DCP Ally Mlege aliyekuwa Makao Makuu ya Polisi amehamishiwa Kanda Maalumu ya Dar es Salaam kwenda kuwa Mkuu wa utawala na raslimali watu.
Vilevile, Kamanda wa Polisi mkoa wa Kipolisi Kinondoni, Charles Kenyela amehamishiwa Makao Makuu ya Upelelezi wa makosa ya jinai na nafasi yake inachukuliwa na aliyekuwa Mkuu wa Upelelezi wa makosa ya jinai mkoa wa Arusha ACP Camilius Wambura. Aidha, ACP Duwan Nyanda aliyekuwa Makao Makuu ya Upelelezi anaenda kuwa Mkuu wa Upelelezi wa makosa ya jinai Mkoa wa Arusha.
Uhamisho huo ni wakawaida kwa mujibu wa kanuni, taratibu na miongozo ya Jeshi la Polisi.
Imetolewa na:
Advera Senso-SSP
Msemaji wa Jeshi la Polisi (T).
0 comments:
Post a Comment