mwili wa kichanga hicho kilichotupwa katika dampo baada ya kutolewa kwenye dampo hilo
Mwenyekiti wa serikali ya mtaa wa Kota Mlandege Bi Mida Mkwawa akielezea tukio hilo
Wananchi wakishuhudia tukio hilo
Tunaomba radhi kwa picha hii.........mwili wa mtoto huyu baada ya kutolewa katika dampo
Polisi wakiwasili eneo la tukio
Mwenyekiti wa serikali ya mtaa wa kota Mlandege akitoa maelezo kwa askari polisi
Matukio ya wanawake kutupa watoto
yameendelea kuchukua kasi katika Manispaa ya Iringa kufuatia
mwanamke mwingine mmoja mkazi wa kata ya Mlandege katika Manispaa ya Iringa
kumtupa mtoto wake katika dampo la kuhifadhia taka usiku wa kuamkia
leo.
Wakizungumza katika na dampo alipotupwa kichanga hicho baadhi ya wananchi wamesema kuwa mtoto huyo mchanga anadaiwa kutupwa
usiku wa kuamkia leo.
Wananchi hao wamesema kuwa upo
uwezekano wa mwanamke aliyetenda unyama huo kukamatwa iwapo
wananchi watatoa ushirikiano na kumfichua mhusika.
Kwani wamedai kuwa ni vigumu mwanamke kutoa mimba na kutupa kiumbe hicho katika dampo la taka bila kujulikana.
Mwenyekiti wa serikali ya mtaa wa kota
kata ya Mlandege katika Manispaa ya Iringa Mida Mkwawa mbali ya
kuthibitisha kutokea kwa tukio hilo bado amewataka wananchi
kuungana kumsaka mwanamke anayedaiwa kutenda unyama huo.
Mkwawa amesema amepokea
taarifa kutoka kwa wananchi wasamaria wema kuhusu kutupwa kwa
mtoto huyo ndani ya dampo la taka katika eneo hilo.
Hata hivyo amesema kuwa katika mtaa
wake hakukuwa na binti mwenye mimba na kuwa yawezekana kabisa
mhusika wa tukio hilo ametoka nje ya mtaa huo na kuwataka wananchi
wa mitaa mbali mbali ya mji wa Iringa ambao walipata kumshuhudia
binti yeyote akiwa na mimba na sasa hana mimba kutoa taarifa polisi.
Hata hivyo taarifa zisizo rasmi ambazo mtandao huu umezipata zinadai mwanamke huyo amepatikana. Taarifa zaidi endelea kufuatilia mtandao huu.
0 comments:
Post a Comment