Ndege zote aina ya Boeing 787 Dreamliner
zimesimamishwa hadi pale matatizo yanayoweza
kusababisha moto yatakapokuwa yamepatiwa
ufumbuzi.
Nchi mbali mbali zikiwemo Chile, India, Qatar,
Ethiopia na Umoja wa Ulaya zimefuata hatua ya
Marekani, baada ya ndege mbili za aina hiyo
zinazomilikiwa na shirika la ndege la Japan kutua
katika hali ya dharura Jumatano.
Wataalam wanakadiria kuwa itachukua muda wa wiki
kadhaa kurekebisha makosa katika ndege hiyo ya
kimarekani iliyotengenezwa kwa teknolojia ya hali ya
juu.
Mkurugenzi Mkuu wa kampuni ya Boeing Jim
McNerney amesema kuwa kampuni hiyo inasikitishwa
na usumbufu uliotokana na hitilafu hizo, na kuahidi
kufanya kila juhudi kulimaliza tatizo hilo haraka.
0 comments:
Post a Comment