Lance armstrong
Bingwa wa zamani wa mbio za baskeli maarufu kama Tour
de France, Lance Armstrong amekiri kutumia madawa za
kumuongezea nguvu, katika mahojiano na mtayarishaji wa
vipindi vya kijamii katika televisheni, Oprah Winfrey.
Alipoulizwa na Oprah kama alitumia madawa ili kushinda
mbio hizo, kwa mara ya kwanza Armstrong alisema ''Ndio''.
Armstrong alikiri kuwa bila matumizi ya dawa hizo
asingeweza kushinda mbio hizo mara saba. Lance
Armstrong alivuliwa mataji yake yote baada ya shirika la
kimarekani la kupambana na matumizi ya madawa katika
michezo kutoa ripoti yake mwezi Oktoba mwaka jana.
Armstrong alipigwa marufuku kushiriki katika michuano, na
kupoteza udhamini wote kwa fuko lake la Livestrong,
alilolianzisha kupambana na ugonjwa wa saratani.
dwswahili
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment