Taifa
Stars imewasili leo hapa Marrakech, Morocco tayari kwa mechi ya mchujo
ya Kombe la Dunia dhidi ya wenyeji Morocco itakayochezwa Jumamosi- Juni 8
mwaka huu.
Stars
inayodhaminiwa na Kilimanjaro Premium Lager imefikia hoteli ya Pullman
ambayo pia ilifikia timu ya Ivory Coast ilipokuja kucheza na Morocco.
Stars imetua na kikosi cha wachezaji 21 wakati Mbwana Samata na Thomas
Ulimwengu watawasili kesho- Juni 4 mwaka huu saa 8 mchana wakitokea
Maputo, Msumbiji ambapo jana- Juni 2 mwaka huu timu yao ya TP Mazembe
ilicheza mechi ya Kombe la Shirikisho.
Mechi kati ya Stars na Morocco itachezwa kuanzia saa 3 usiku kwa saa za hapa ambapo Tanzania itakuwa saa 5 usiku.
Boniface Wambura
Ofisa Habari Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)
+212610120619
Marrakech, Morocco
0 comments:
Post a Comment