Main Menu

Monday, June 17, 2013

TIMU ZA TAIFA ZA ETHIOPIA, TOGO NA EQUATORIAL GUINEA HATARINI KUNYANG'ANYWA POINI.

Timu za soka za mataifa ya  Ethiopia, Togo na Equatorial Guinea zipo kwenye hatari ya  kukubwa na adhabu ya kunyang’anywa alama tatu katika michezo yao ya kufuzu kwa kombe la dunia kutokana na kutumia wachezaji wasiokuwa na sifa.

Taarifa ya Fifa imeeleza kuwa Ethiopia ambayo jana ilifunga na  Afrika ya kusini goli 1 kwa 1 na kuongoza kundi A inatuhumiwa kumtumia mchezaji asiyestahili katika mchezo wao na Botswana juni 8 na Ethiopia kushinda magoli 2 kwa 1.

Aidha Togo itachunguzwa kama ilimtumia mchezaji asiyetakiwa katika mchezo dhidi ya Cameroon katika kundi I uliochezwa juni 9 wakati Equetorial Guinea itakuwa ikichunguzwa katika ushindi wao wa magoli 4 kwa 3  dhidi ya Cape Verde uliochezwa march 24 mwaka huu.

Sheria za Fifa zinaruhusu nchi kutumia mchezaji mwenye asili ya taifa husika aliyeishi kwa kipindi kisichopungua miaka mitano na taifa litakalo bainika kwenda kinyume na kipengele hicho litanyang’anywa ushindi kwenye michezo aliyecheza nyota husika.

0 comments:

Post a Comment