Mwenyekiti wa chama cha Demokrasia na Maendeleo Chadema nchini Tanzania,
Freeman Mbowe, amevituhumu vyombo vya dola kuwa, vinawafahamu watu
waliohusika na mlipuko wa bomu uliotokea juzi katika viwanja vya Soweto
kwenye mkutano wa chama hicho.
Mbowe, amesema tukio hilo ni la kisiasa
na lilipopangwa awali. Amesema wamegundua risasi za bunduki aina ya SMG
na bastola zilitumika mara baada ya mlipuko huo jambo linalozusha hofu
na kuhatarisha demokrasia ya vyama vingi nchini tanzania.
Kwa upande
wake Mkuu wa Jeshi la Polisi (IGP), Said Mwema ameunda timu
itakayoongozwa na makamishna wawili, kwenda mkoani Arusha kuongeza nguvu
ya uchunguzi wa tukio hilo.
Mbowe amesema ni bora serikali itangaze
kuachana na mfumo wa vyama vingi kuliko kuruhusu mauaji na vurugu katika
mikutano ya vyama vya upinzani vinavyoonekana kutoa wakati mgumu kwa
watawala.
Amesisitiza kuwa, uchunguzi wa awali katika eneo la tukio
umebaini kuwa bomu lililolipuliwa ni la kiwandani na si la kutengenezwa
kwa mikono.
Wakati huo huo serikali imetoa tamko kuhusu mlipuko huo uliotokea mkoani arusha siku ya jumamosi katika mkutano wa kuhitimisha kampeni za uchaguzi wa viti vya udiwani uliofanyika jana.
Akitoa kauli hiyo Bungeni waziri wa nchi ofisi ya rais sera, uratibu na Bunge Wiliam Lukuvi amesema serikali haita vumilia vitendo hivyo vya uvunjifu wa amani na kuahidi zawadi ya shilingi milioni mia moja kwa mtu yeyote atakayewezesha kukamatwa kwa waalifu hao.
Hata hivyo Lukuvi amwailaumu viongozi wa vyama vya siasa kwa kuwajengea chuki polisi kwa wanachama wake hali iliyochangia polisi kushindwa kumkamata mtuhumiwa baada ya wananchi kuanza kuwashambulia polisi baada ya mlipuko huo.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment