Monday, June 17, 2013
SPAIN, ITALY ZAANZA VIZURI MICHUANO YA SHIRIKISHO NCHINI BRAZIL.
pedro akishangilia bao lake huku akifuatwa na sergio ramos
katika michuano ya kombe la mabara, Confederations Cup , michuano inayofanyika nchini Brazil Uhispania jana ilianza vizuri kampeni yake kwa kuiangusha Uruguay kwa mabao 2-1 .
Pedro na Roberto Soldado walipata mabao mapema katika kikosi cha kocha Vicente del Bosque, timu ambayo ilipaswa kupata mabao mengine zaidi.
Luis Suarez aliipatia Uruguay bao la kufutia machozi dakika mbili kabla ya mpira kumalizika.
Nae Mario Balotteli aliipatia timu ya Italia bao la ushindi wakati Italia ilipoizaba Mexico kwa mabao 2-1.
Bao la kuongoza la italy lilifungwa na kiungo mkongwe pirlo.
Leo ni zamu ya Nigeria ambayo inapambana na Tahiti .
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment