Mkuu wa majeshi ya Tanzania Mheshimiwa Kaimu Davis Mwamunyange, alifanya ziara ya Kikazi nchini Oman kuanzia tarehe 23 hadi 27 Juni 2013 kwa Mwaliko wa mwenyeji wake Luteni Jenerali Ahmed bin Harith Al Nabhani.
Ziara hii ilikuwa na madhumuni makuu ya kuimarisha uhusiano wa kindungu uliopo baina ya Oman na Tanzania kupitia sekta ya ulinzi na kuanzisha uhusiano wa karibu na ushirikiano baina ya vyombo hivi vya ulinzi kati ya Tanzania na Oman.
Katika ziara hii Mhe. Jenerali Mwamunyange alikutana na kufanya mazungumzo na Mwenyeji wake Luteni Jenerali Ahmed bin Harith Al Nabhani na pia kukutana na Waziri katika Ofisi ya Mfalme Mheshimiwa Luteni Jenerali Sultan bin Mohamed Al Nuamani .
Mbali na kukutana na viongozi hawa wa Oman, Mkuu wa majeshi alipata nafasi kutembelea maeneo kadhaa kujonea shughuli mbalimbali za Jeshi la Oman, alitembelea makumbusho ya Jeshi la Oman, Chuo cha Uongozi na kamandi cha Oman, Chuo cha Jeshi la Anga, Hospital ya Jeshi , Makao makuu ya Jeshi la Askari wa Miguu pamoja Makao makuu ya Jeshi la Majini.
Katika maeneo yote aliyotembelea Mheshimiwa Mkuu wa Majeshi alifurahishwa sana na shughuli za jeshi la Oman na kuridhika na hatua iliyopigwa na Jeshi la Oman.
Mkuu wa majeshi pia alitembelea ofisi za Ubalozi wa Tanzania nchini Oman kujionea shughuli mbalimbali za Ubalozi na pia kuhudhuria hafla ya chakula cha Usiku kilichoandaliwa kwa heshima yake nyumbani kwa Mheshimiwa Balozi
Mkuu wa majeshi pia alitembelea ofisi za Ubalozi wa Tanzania nchini Oman kujionea shughuli mbalimbali za Ubalozi na pia kuhudhuria hafla ya chakula cha Usiku kilichoandaliwa kwa heshima yake nyumbani kwa Mheshimiwa Balozi
Mkuu wa Majeshi Jenerali Davis Mwamunyange akikagua Gwaride la Mapokezi mara alipowasili katika Makao makuu ya Jeshi la Oman kuanza Ziara ya kikazi nchini Oman, kushoto ni Mkuu wa Majeshi ya Oman Luteni Jeneral Ahmed bin Harith Al Nabhani.
0 comments:
Post a Comment