Timu ya Manchester United imeendeleza
ushindi katika michezo ya kujiandaa na msimu mpya wa ligi kuu nchini England baada
ya kuichapa timu ya san jose mabao 3-1 katika Uwanja wa Avaya mjini San Jose
nchini marekani.
Kiungo Juan Mata ndiye alianza
kuifungia United asubuhi ya leo katika dakika ya 32, kabla ya Memphis Depay kufunga
la pili dakika ya 37.
San Jose walifanikiwa kupata bao lao
dakika ya 42 kupitia kwa Fatai, chipukizi Andreas Pereira aliifungia man u bao
la kichwa na kuihakikishia ushindi timu hiyo.
Kikosi cha Louis van Gaal sasa
kitamenyana na mabingwa wa Ulaya, Barcelona katika mchezo ujao wa michuano ya
Kombe la Mabingwa wa Kimataifa Jumamosi nchini humo.
Kikosi cha Manchester United
kilikuwa; kipindi cha kwanza; Johnstone, Darmian, Jones, Blind, Shaw, Carrick,
Schneiderlin, Young, Mata, Memphis na Rooney.
Kipindi cha pili: Johnstone, McNair,
Smalling, Evans, Blackett, Lingard, Schweinsteiger, Herrera, Pereira, Januzaj
na Wilson.
0 comments:
Post a Comment