Timu ya Taifa ya Wanawake ya Tanzania wenye umri chini ya
miaka 20 (Tanzanite) wanatarajiwa kuondoka kesho jumatano asubuhi kwa Rwanda
Air kuelekea nchini Zambia kwa ajili ya mchezo wa marudiano dhidi ya Young
She-Polopolo.
Tanzanite inayowania kufuzu kwa Fainali za Kombe Duniwa
mwaka 2016 nchini Papua New Guinea, itacheza mchezo huo wa marudano siku ya
jumamosi tarehe 25 Julai, jijini Lusaka.
Katika mchezo wa awali uliofanyika takribani wiki mbili
zilizopita, Tanzanite ilipoteza mchezo wake nyumbani baada ya kufungwa kwa
mabao 4 – 0, hivyo kuhitaji kushinda zaidi ya mabao 5 – 0 ili kuweza kusonga
katika hatua inayofuata.
Msafara wa Tanzanite utaongozwa na Mjumbe wa Kamati ya
Utendaji ya TFF, Blassy Kiondo utajumuisha makocha Rogasian Kaijage (kocha
mkuu), Edna Lema (kocha msaidizi), Peter Manyika (kocha wa makipa), Christina
Luambano (Daktari), Mwanahamis Abdallah (mtunza vifaa) na Meneja Furaha Francis.
Wachezaji watakaosafiri ni Stumai Abdallah, Shelder
Boniface, Donisia Minja, Najiat Abbas, Neema Kiniga, Happyness Mwaipaja, Jane
Lucas, Anastazia Katunzi, Anna Mwaisura, Janet Pangamwene, Gelwa Rugomba,
Blandina Ambros, Amina Ramadhan, Asha Shaban, Maimuna Hamis, Zuwena Hamis,
Amisa Athuman na Wema Richard.
0 comments:
Post a Comment